Unknown Unknown Author
Title: Usijidanganye Mwaka 2018 Kwa Kujiambia Maneno Haya Mawili
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio? Hongera kwa kuuanza mwaka mpya wa 2018, Ni imani yangu kuwa utaenda kuitum...

Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio?

Hongera kwa kuuanza mwaka mpya wa 2018,
Ni imani yangu kuwa utaenda kuitumia vizuri sana nafasi hii ya pekee kwako katika kuweka juhudi kubwa ili kuweza kufikia mipango yako ya mwaka 2018.

Binafsi mwaka huu nitakwenda kuweka juhudi kubwa sana ambayo nina hakika itakuwa na matokeo yaliyo makubwa sana kwangu.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye kwa moyo mkunjufu kwenye makala yetu ya leo ya siku ya kwanza kwa mwaka huu 2018,
Ambapombapo nitakwenda kukushirikisha maneno ambayo yamekuwa yakiwadanganya wengi hasa kwenye siku hizi za mwazo wa mwaka ambapo wengi wamekuwa na hamasa kubwa ya kuupokea mwaka na hivyo kuitumia nafasi hiyo na hamasa hiyo katika kuweka mipango yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiambia maeneo haya na kuona basi yanaweza kuleta mabadiliko makubwa pasipo wao kuwajibika lakini mpaka wanamaliza mwaka wanajikuta hakuna hatua waliyo piga zaidi ya kuongezeka kwa Umri wao.

MWAKA MPYA NA MAMBO MAPYA,
Bila shaka nawe rafiki yangu ulisha wai kujidanganya kwa kujiambia maneno hayo na kuendelea kusubili maneno hayo yakulete mambo mapya,
Maneno hayo ni mkumbo tu ambao unafuatwa na watu wengi lakini ni maneno ambayo hayana ukweli wowote iwapo wewe hauta amua kuwa mtu mpya.

Kinacho badilika ni namba 2017->2018,
Vipi usipo badilika wewe?
Nini kitakuwa kipya kwa mwaka mpya?
Au nini kitakuwa kipya kwa kuishi mazoea ya mwaka ulio pita?.

Sipendi wewe rafiki yangu ujidanganye Wala sipendi wewe rafiki yangu uwadanganye watu kwa kukufuata wewe,
Badala yake wewe uwe sehemu ya mabadiliko kwa mwaka 2018 ambayo yatakuwa na matokeo makubwa.

Unawezaje kubadilika 2018?

Zipo njia nyingi sana sahihi zinazo weza kutengeneza mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako kwa mwaka 2018,
Njia hizi zitafanya kazi kwa wewe kuchukua maamuzi yaliyo sahihi.
Maamuzi unayo weza kuchukua ili kuhakikisha mwaka unakuwa ni wewe mabadiliko kwako ni pamoja na hizi zifuatazo.

1.Acha kuongea,Fanya kwa vitendo,
Watu wengi ni waongeaji wa maneno pasipo vitendo lakini wewe rafiki yangu kuwa kinyume na hao wote ili uweze kuwa mpya kwa mwaka 2018.
Anza kufanya kwa vitendo kwa sababu vitendo vina matokeo makubwa zaidi kuliko maneno yasiyo na vitendo.

2.Anza kusoma vitabu na Kufanyia kazi yale unayo jifunza,
Kati ya njia zote zenye nguvu kubwa ya kubadili maisha ya watu basi ni kusoma vita,Unapo soma vitabu unakuwa umejipa nafasi kubwa ya kuishi Uzoefu wa maisha ya mwandishi wa kitabu hicho lakini haitakuwa kigezo cha wewe kupiga hatua unatakiwa kufanyia kazi yale unayo jifunza kwa juhudi kubwa.

3.Acha kuishi Mazoea,
Kama ulikuwa unafanya mambo yale yale kwa njia zile zile bila shaka ulipata matokeo ya kawaida sana kwenye maisha yako,
Hatua unayo paswa kwenda kuchukua sasa ni kuacha kufanya kwa mazoea na Anza kufanya mambo mapya kwa njia mpya na utapata matokeo mapya.

4.Anza kuudhuria semina mbalimbali,
Zipo semina nyingi sana ambazo zinaendeshwa sehemu mbalimbali ambapo sipo semina za bure na hata za kulipia hivyo anza kuudhuria semina kwa namna yoyote nina hakika utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.

5.Ondoka kwenye mfumo hasi wa maisha kisha Hamia kwenye mfumo chanya wa maisha,
Hapo kuna zoezi zito sana ambapo unatakiwa kuliweka ili kuweza kupata matokeo mazuri hii ni kwa sababu ni rahisi sana kuishi kwenye mfumo hasi wa maisha kuliko kuishi mfumo chanya pia hata unapo hamia kwenye mfumo chanya bado inaweza kuwa rahisi sana kurudi kwenye mfumo hasi hivyo kuwa makini sana sana.

Kwa kufuata mambo hayo matano na mengine yanayo fanana na hayo utakuwa tayari upo kwenye nafasi nzuri ya wewe kuwa mwingine kwa mwaka huu na hata miaka yote inayo endelea kwenye maisha yako.

Epuka kabisa kosa nililo kushirikisha hapo juu ambalo limekuwa likiwa poteza wengi na kushindwa kufikia mipango wanayo kuwa wamejiwekea kwenye maisha yao.

Kwa mwaka 2018 ninakwenda  kuanzisha program maalumu kwa watu maalumu,
Watu ambao wanapenda kujifunza na Kuchukua hatua kwenye maisha yao lakini kutokana na changamoto mbalimbali wamekuwa wanashindwa kabisa kufikia mipango ya maisha yao.

Hivyo nitakuwa na programu maalumu ya kuwa simamia watu hao kwa ukaribu mkubwa sana ili waweza kupiga hatua kubwa kwa mwka 2018.
Nikukaribishe wewe rafiki yangu na nitapenda kuona unanufaika sana na program hii kwa mwaka 2018.

Kuweza kujiunga na program hii wasiliana nami kwa simu 0715222989/errynine6@gmail.com WhatsApp.

Karibu sana na rafiki yangu,
Na wako rafiki katika mafanikio
Ernest Lwilla.
Contact:0 715222989/errynine6@gmail.com

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top