Unknown Unknown Author
Title: Programu Maalumu Kwa Watu Maalumu 2018.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio? Unaendeleaje na harakati zako za kila siku kuhakikisha unaendelea kusonga m...

Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio?
Unaendeleaje na harakati zako za kila siku kuhakikisha unaendelea kusonga mbele zaidi kimafanikio?

Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya na unaendelea vema katika kuweka juhudi ili kuendelea kufanya maisha yako kuwa bora zaidi kila siku.

Ikiwa ni siku chache tangu tuuanze  Mwaka wetu wa mafanikio 2018 ninahakika kubwa ya kuwa umesha weka mipango yako vizuri tayari kwa kwenda kufanyia kazi.
Karibu kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha yale muhimu niliyo jifunza kwa ndugu rafiki na jamaa ambao nimekuwa karibu nao kwa mwaka mzima ulio pita huku tukiwa tunashauriana mambo mbalimbali ili kuhakikisha maisha yetu yanakuwa bora zaidi ya jana.

Tangu 2016 nimekuwa nikishirikiana na kuwasiliana na watu wengi sana wakini shirikisha hasa changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakizipitia kwenye hatua mbalimbali za maisha yao ya mapambano,
Ambapo changamoto kubwa ili kuwa ni kushindwa kufikia mipango wanayo kuwa wamejiwekea kwenye maisha yao na hivyo kutokana na hilo nilitoa ushauri kwa watu wengi namna ya kuipita changamoto hiyo na wengi walio fanyia kazi ushauri huo walipata matokeo makubwa sana yaani walipiga hatua kubwa sana lakini hiyo ni kwa watu wachache sana sana tofauti na idadi ya watu nilio wasiliana nao kwa kipindi hicho.

Changamoto kubwa kwa watu wengi sio kuweka malengo,mipango au mikakati ya kwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima,
Changamoto kubwa ni pale wanapo Anza kuchukua hatua ili kuweza kutekeleza malengo na mipango yao hapo ndio wengi hukwamishwa na changamoto na kurudi kuendelea kuishi maisha ya kawaida au ya mazoea.

Watu wengi mwanzoni mwamwaka wamekuwa wakitumia muda huo na hamasa zao kuweka malengo na mipango yao mikubwa sana,
Lakini kuitekeleza mipango hiyo hapo ndio imekuwa changamoto kubwa kwa sababu wanapo Anza kufanyia kazi mipango hiyo inakutana na changamoto nyingi ambazo mala nyingi zinakuwa kuzuizi kwao kupiga hatua.
Mfano;Mtu ana mpango mzuri anahitaji kuukamilisha ndani ya kipindi cha mizezi 6 na anachukua hatua kweli lakini akiwa katikati ana kutana na changamoto nyingi ambazo hazimpi nafasi tena kuendelea kuweka juhudi kubwa na hivyo kukatishwa tamaa na kuishia hapo hapo na kujidanganya kuwa watafanya tena mwakani.

Kutokana na hilo mimi rafiki yako nimeanzisha programu maalumu kwa watu maalumu 2018.

Watu hao ni nani?

1.Watu hao ni wewe rafiki yangu ambae umekuwa unakwamishwa na changamoto hizo kuweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
2.Watu hao ni wewe rafiki yangu unae Penda kujifunza na kufanyia kazi yale unayo jifunza lakini hupigi hatua kabisa.

Kitu gani utakipata zaidi kwenye Programu hiyo maalumu 2018?

Kama nilivyo kwambia hapo juu kuwa changamoto kubwa kwa watu sio kuweka malengo,Changamoto ni kukamilisha kile wanacho kuwa wamepanga kufanya,
Hivyo mimi rafiki yako nitakwenda kukushirikisha maarifa mziri sana ambayo yatakuwezesha kufikia malengo hayo kwa kiwango cha juu sana.

Nitakwenda kukusimamia kwa karibu sana kwenye kila hatua utayo taka kupiga,
Nitakuwa nawe bega kwa bega kuhakisha unapiga hatua kubwa 2018.

Ni maarifa gani ya tofauti nitakayo jifunza kwenye programu hii 2018?

Nitakwenda kushirikisha masomo mbalimbali yanayo kuwezesha kuwa imara kwenye kila nyanja ya maisha yako,
Nitafundisha Msingi muhimu wa maisha ya mafanikio ambao ndio msingi ninao uishi mimi,Nitakushirikisha Kanuni nzuri ya kuweka Akiba hata kama kipato chako ni kidogo sana,Nitakwenda kukushirikisha njia bora inayo wawezesha matajiri kuendelea kuwa tajiri,Nitakwenda kukushirikisha Elimu kubwa kuhusu fedha,Nitakwenda kukushirikisha masomo mazuri ya biashara,Nitakwenda kukushirikisha masomo mazuri ya Uwekezaji,Nitakwenda kukushirikisha njia bora ya kutunza akiba zako kidogo kodogo n.k kimsingi hata utajifunza kila kitu kitakacho kuwa na mchango mkubwa kwako kupiga hatua kubwa mwaka 2018.

Kwanini usitushirikishe maarifa hayo kwenye Ukulasa huu na kila mmoja akaweza kujifunza?

Ni kweli nina weza kufanya hivyo vizuri,
Lakini kama nilivyo kwambia nimekuwa nikiwasiliana na kushauri watu wengi kwa mda mwingi lakini wanao Fanyia kazi ushauri na Maarifa ninayo washikisha ni wachache sana,
Hii inatokana na kwamba ushauri na Maarifa hayo makubwa ninayo wapa BURE hawafanyi kazi licha ya mimi kuyapata kwa ghalama kubwa sana sana.

Kwani maarifa hayo ndiyo yatakayo kamilisha mipango yangu mwaka 2018?

Hapana,
Maarifa hayo yatakuwasaidia kuweza kufanya kazi kwa ubora sana na kupata matokeo yaliyo bora zaidi.
Maarifa hayata fanya kazi pekee yake ni lazima wewe uweke juhudi na Maarifa nitakayo kupa yatakuwa msingi imara kwako katika kupiga hatua zaidi.

Ahadi yangu kwako rafiki 2018.
Kama nilivyo kwambia natoa ghalama kubwa sana kuyapata maarifa haya ikiwa ni pamoja kuwalipa makocha na walimu mbalimbali wanao nisimamia mimi kwa ukaribu ili kuweza kupiga hua kubwa,
Hivyo ni hasara kubwa sana kwangu iwapo nitakufa na Maarifa hayo mazuri wakati wewe rafiki yangu umekwama na unahitaji msaada wa thati kuweza kupiga hatua zaidi.

Na wewe unasimamiwa?

Ndiyo,
Mimi nina kocha na walimu wanao nisimamia ili niweze kupiga hatua kubwa mfano:Ninakocha wangu anae endesha  huduma hii kwenye KISIMA CHA MAARIFA ,
Hivyo nawe rafiki yangu huwezi kupiga hatua kirahisi pekee yako ni lazima uwe na mtu utakae fanya nae kwa ukaribu na mtu huyo ni mimi rafiki yako Ernest.

Karibu sana rafiki yangu tuweze kupiga hatua pamoja kwa mwaka 2018 kwa kufanya kazi pamoja.
Nitakwenda kukushirikisha mambo mengi sana ambayo nimekuwa nikiyaishi kwenye maisha yangu yote.

Karibu kwenye PROGRAM MAALUMU KWA  WATU MAALUMU 2018.
Kupata utaratibu wa namna ya kuipata huduma hii wasiliana nami moja kwa moja  kwa WhatsApp namba 0715222989/errynine6@gmail.com
Hapo utaweza kupata utaratibu wote wa program hii maalum 2018.

Na wako rafiki/kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla.
Karibu sana rafiki yangu.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top