Unknown Unknown Author
Title: Huu Ndio Utumwa Pekee Unao Zika Ndoto Za Watu Wengi Duniani
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki yangu? Unaendeleaje na mapambano ya kuhakikisha mwaka huu unakuwa na mafanikio makubwa kwako? Ni imani yangu kubwa kuwa wewe...

Habari rafiki yangu?
Unaendeleaje na mapambano ya kuhakikisha mwaka huu unakuwa na mafanikio makubwa kwako?

Ni imani yangu kubwa kuwa wewe ni mzima wa afya njema kama ilivyo kwangu,
Ambapo ninaendelea vema kabisa na shughuli zangu zote kwa kuweka juhudi kubwa zaidi ili kuhakikisha mwaka huu napiga hatua kubwa zaidi.

Karibu sana rafiki yangu kwenye makala hii ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha utumwa mkubwa unao zika ndoto za watu wengi sana Dunia,
Hivyo wewe rafiki yangu ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye mwaka huu ni lazima uondoke haraka sana kwenye utumwa huo na baada ya kuondoka kwenye utumwa huo utapiga hatua kubwa zaidi kwenye maisha yako.

Awali kabisa Nianze kwa kisema,
Huwezi kwa kufikia mafanikio makubwa kwa kuweka nguvu na juhudi yako pekee,Huwezi kufikia mafanikio makubwa kwa kufanyia kazi masaa 24 pekee ambayo kila mmoja wetu anapewa kila siku pia Huwezi kufikia mafanikio makubwa kwa kutegemea fedha yako pekee tuu na iwapo utafanya hayo yote basi sahau kabisa kuhusu mafanikio kwa sababu ni zoezi gumu sana kufanikiwa kwako ila sio ndio ukate tamaa ya kuendelea kufanya kazi.

Rafiki upo utumwa wa aina nyingi ambao mtu unaweza kusema labda kuna mtu ameusababisha kwako lakini utumwa huu ninao kwenda kukushirikisha leo Wewe ndie umeamua kuwepo hapo na wewe ndie unae weza kuondoka kwenye utumwa huo.

Rafiki utumwa ninao uzungumzia hapa ni MFEJI MMOJA WA KIPATO,
Kwenye makala zilizo pita nilishawai kukushirikisha hii kwa kina sana lakini naona bado ni tatizo kwa watu wengi na hivyo kuendelea kuwa tegemezi wa mkondo mmoja wa kipato jambo ambalo ni hatari zaidi na hali kupi uhuru wa kifedha.

Kutegemea mfereji mmoja tu wa kipato ni aina ya ugonjwa hatari na wenye madhara makubwa sana kwa watu,
Ivi vipi mfereji huo wa kipato unapo patwa na changamoto?
Vip mfereji huo mmoja unapo kauka kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako?

Bahari haijawai kukauka kwa sababu inakuwa ni mifereji mingi inayo peleka maji kwenye bahari hiyo,
Sasa ili na wewe rafiki yangu usiweze kupata shida yoyote hasa mkondo mmoja wa kipato unapo kauka ni muhimu kuwa na mifereji mingi ya kipato.

Unapo fikia hatua hii ya kuwa na mifereji zaidi ya mmoja wa kipato hapo unakuwa upo huru kwa sababu hata inapo tokea mfereji mmoja kupatwa na changamoto basi unakuwa na uhakika wa kuendelea kuzalisha zaidi kwenye mfereji mwingine.

Hatua ya kuwa na mifereji mingi ya kipato inakupa uhuru wa wewe kufanya kazi kwa kiwango cha juu sana kwa sababu Unakuwa hauna hofu yoyote kuhusu kipato.

Ukweli kuhusu mkondo mmoja wa kipato,
Kwanza tunaishi  kwenye hali ambayo haitabiliki kabisa kiuchumi kiasi kwamba Unaweza kulala na kazi na kuamka huna kazi,Unaweza kulala na biashara inayo kulipa sana na kuamka na biashara yenye ushindani mkali kiasi kwamba huwezi kuwa na uzalishaji mkubwa wa kipato,Unaweza kulala na fedha nyingi sana lakini unaamka imesha shuka thamani yake au Hata umelala na mzunguko mkubwa wa fedha na kuamka na mzunguka ambao hauwezi kukupa maisha bora kwako,
Hayo yote ni mambo ambayo tunayo kwenye maisha yetu ya kila siku hivyo tusipo ujua ukweli bado itakuwa hatari sana kwetu.

Unapo kuwa na mifereji mingi ya kipato kuna kuwa na faida nyingi sana kwako Mfano:Kutumia muda wa watu wengine hii ni kwa sababu huwezi kusimamia shughuli zote wewe mwenye hivyo kwa kuajiri wengine inakuwa faida kwako pia Kuwa na mifereji mingi ya kipato inakuwa ni salama kwako kwa sababu Unakuwa na uhakika wa kuzalisha kila siku.

Hivyo rafiki kuondokana na utumwa huu wa mfereji mmoja wa kipato ni muhimu kuanza kuona ni thamani gani nyingine unayo weza kutoa kwa wengine nao wakawa tayari kulipia thamani hiyo,
Kwa kufanya hivyo unakuwa tayari na mfereji mwingine wa kipato ambao utakusaidia kuondoka kwenye utumwa wa kutegemea mfereji mmoja wa kipato.

Kwa ushauri napendekeza uwe na mifereji angalau kwanzia miwili,mitatu na kuendelea,
Lakini unapo chukua hatua hiyo ya kwenda kuwa na mifereji mingi ya kipato ni muhimu kuhakikisha mifereji mingine imesha kuwa na uzalishaji mzuri na imesha anza kukupa faida nzuri.
Usianzishe mifereji mingi kwa wakati mmoja hata kama unao uwezo wa kufanya hivyo hii ni kwa sababu kusimamia biashara Au huduma zaidi ya moja ni kazi ngumu sana na hivyo kwa mwanzo linaweza kuwa zoezi gumu kwako kwa sababu Unakuwa hauna uzoefu wa kutosha.

Mwisho kabisa rafiki yangu Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye programu maalumu kwa watu maalumu 2018 ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kwa ukaribu zaidi,
Ambapo nitakwenda kufundisha masomo mengi sana yatakayo kuwezesha kupiga hatua kubwa kwa mwaka 2018.

Karibu sana rafiki yangu ili kupata taarifa na utaratibu wa kujiunga na program hii wasiliana nami moja kwa moja kwa namba WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com.

Karibu sana sana na tuweze kufanya kazi pamoja na tupige hatua pamoja 2018 na kufanya kuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwetu.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top