Unknown Unknown Author
Title: Hiki Ndio Kitu Pekee Usicho Kijua Kuhusu Fedha.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio? Unaendeleaje na mapambano? Ni imani yangu kubwa kuwa unaendelea vizuri kam...

Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mfanikio?

Unaendeleaje na mapambano?
Ni imani yangu kubwa kuwa unaendelea vizuri kama ilivyo kwangu.

Ikiwa ni siku nyingine nzuri kwetu ni Fursa ya pekee kwetu kwenda kuitumia vizuri siku  hii ya leo ili kutuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu na hivyo kuweza kuwa na maisha yaliyo bora.

Nichukue nafasi hii ya pekee kukukaribisha wewe rafiki yangu kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo kubwa usilo lijua kuhusu fedha,
Kama unavyo jua fedha ndio changamoto kubwa sana kwa watu wengi kwanzia kuipata na mpaka kwenye kuitumia.

Watu wanapenda kufanikiwa na wanahakiki kubwa ya kufanikiwa lakini jambo wasilo lijua ni kwamba huwezi kufanikiwa kwa kukazana wewe pekee yako,
Hivyo rafiki jambo hili ninalo kwenda kukushirikisha ndilo litakuwezesha wewe kupiga hatua zaidi mpaka kufikia mafanikio makubwa na hata utajiri.

Jambo kubwa usilo lijua fedha ni KUIWEKEZA FEDHA UNAYO PATA ILI KUIZALISHA ZAIDI,
Haijalishi kipato chako ni kikubwa au nikidogo lakini jambo unalo takiwa kufanya ni kuwekeza,
Unapo wekeza unakuwa unatumia fedha kuzalisha fedha zaidi hata kama ni kiwango kidogo kiasi gani.

Kama unavyo jua uimara wa mti mkubwa sana unategemea mizizi,
Hivyo ndivyo ilivyo hata kwa upande wa jeshi ili liweze kushinda lazima liwe na idadi kubwa ya watu na liwe na kiwango kikubwa cha maandalizi.

Hivyo rafiki jnapo Wekeza zaidi unakuwa sana na mtu anajiimarisha zaidi,Unapo wekeza zaidi unakuwa unaongeza idadi ya ufanyaji kazi wako kwa sababu kadri unavyo ongeza uwekezaji wako ndivyo unavyo zidi kupiga hatua zaidi kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Utasema siwezi kuwekeza kwa sababu kipato changu ni kidogo mno,
Au kipato changu kinanitosha kula kulala,kulipa kodi na ghalama zingine za maisha hivyo nikiwa na kipato kikubwa nitaanza kuwekeza hapa kifupi huna sababu ya kuwa na kipato kikubwa ndipo uwekeze kwa sababu hata ukiwa na kipato kikubwa bado mahitaji kama hayo hayajawai kukosekana.

Uwekezaji unatakiwa kuuufanya ni wa kiwango kidogo sana kutoka kwenye kipato chako,
Hapa unaweza kuwekeza sehemu ya kumi ya kila kipato unacho kipata lakini ukweli ni kwamba unao hivyo kwa sababu huna utaratibu huo wa kuwekeza sehemu hiyo ya kipato chako.

Sehemu ya kumi inatoka wapi?
Sehemu ya kumi ni pesa unayo takiwa kutenga kwenye kila kipato unacho pata kila siku,kila wiki na  kila mwezi kwa mfano:Kila siku kipato chako ni Tsh 1000 basi sehemu ya kumi ni Tsh 100 tu.
Kwa njia hii mahitaji yako yote yanatakiwa kuwa kwenye sehemu ya tisini yaani kwenye 900 inayo baki.

Au unapata Tsh 15000 kila siku basi sehemu ya kumi ni Tsh 1500,
Hii 1500 haitakiwi kuwa kwenye hesabu yoyote zaidi ya kuwekeza tu.

Mbona 100 au 1500 ni fedha ndogo kuwekeza?

Ni kweli  ni fedha ndogo  sana kwa kuiangalia siku moja au mbili lakini vipi ukitenga 1500 mala siku 30?
Au Ukitenga 100 mala siku 30?
Bila shaka Utakuta inazidi kabisa kwa ile pesa unayo zalisha kwa siku.

Je kiwango hicho cha mwezi yaani 3000 au 4500 ukizidisha mala mwaka mmoja yaani miezi 12 unapata ngapi?
Yaani 300×12=36,000
Au 45000×12=540,000 sasa hiyo ni kwa mwaka mmoja pekee vipi viwango hivyo ukizidisha mala miaka 10?
Huwezi ukaanza kujishangaa?

Sasa kwa kipindi hicho chote inakuwa ni fedha ambayo unazalisha kila siku na kuiwekeza kila siku,
Ikiwa wewe unazalisha kila siku na Fedha hiyo uliyo wekeza nayo inazalisha kila siku vipi huwezi kufikia utajiri mkubwa?
Bila shaka kuna kitu muhimu na kikubwa umejifunza hapo kwenye mfano huo.

Hivyo rafiki ili uweze kufikia mafanikio makubwa sana kifedha ni lazima ujifunze kuwekeza,
Uwe na tabia za kuwekeza kila siku na tabia hiyo ya kuwekeza huwezi kuwa nayo bila kujijengea wewe mwenyewe na kujijengea tabia hiyo ni lazima uanzie hapo ulipo sasa kwa kipato ulicho nacho sasa.

Huwezi kuanza kuwekeza ukipata 100,000 wakati huna tabia hiyo tangu ukiwa na kipato cha chini kabisa.
Hivyo anzia hapo hapo chini ulipo kwa kuwekeza kidogo kidogo.

Iwapo una changamoto zozote kuhusu fedha na maisha kwa ujumla,
Karibu kwenye programu maalumu kwa watu maalumu 2018 ili uweze kufanya kazi moja kwa moja na mimi rafiki yako.

Kipi cha ziada utakipata zaidi kwenye Programu hii kwa mwaka 2018,
Nitafanya kazi nawe na kuikamilisha mipango yako muhimu kwa mwaka huu mzima,
Utajifunza njia nzuri ya kuweka akiba,Utajifunza njia nzuri za usimamizi wa biashara,Utajifunza mambo mengi kuhusu fedha nk maarifa yote hayo ni kwaajili yako rafiki yangu ili uweze kupiga hatua kubwa 2018.

Karibu sana,
Kupata utaratibu wa program hii muhimu kwako wasiliana nami moja kwa moja kwa Simu namba WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com.

Karibu sana.
Rafiki/Kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top