Unknown Unknown Author
Title: Sifa Na Vigezo Unavyo Takiwa Kuwa Navyo Ili Kuweza Kunufaika Na Programu Maalumu Kwa Watu Maalumu Kwa Mwaka 2018.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki yangu? Karibu sana sana Kwenye programu maalumu kwa watu maalumu 2018. Ni hakika kubwa kuwa unaendelea kuweka juhudi kubwa n...

Habari rafiki yangu?
Karibu sana sana Kwenye programu maalumu kwa watu maalumu 2018.

Ni hakika kubwa kuwa unaendelea kuweka juhudi kubwa na kuchukua hatua kubwa zaidi ili uweze kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako,
Hongera sana kwa hilo.

Karibu kwenye makala hii ambapo nitakwenda kukushirikisha vigezo ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ili kuweza kunufaika zaidi na Programu maalumu kwa watu maalumu 2018 kama ambavyo nimekuwa nikiitangaza mala kwa mala.

Kusudi pekee kwa watu wengi kila wanapo anzisha mipango yoyote huwa ni wao kunufaika na fedha kutoka kwa watu watakao u
ikubali mipango hiyo,
Lakini mimi nitakwenda tofauti kidogo na utaratibu huo.
Ambapo shida yangu na shauku kubwa niliyo nayo ni kuona nakuwa sababu kubwa kwa watu wengine kupiga hatua na sio kupata fedha.

Shida yangu kwako rafiki yangu sio fedha yako unayo ipata kwa shida kubwa,
Shida yangu na furaha yangu ni kuona wewe unapiga hatua kubwa kwenye maisha yako kwa kushirikiana na mimi rafiki yako hiyo ndiyo furaha na kusudi langu lilipo na kutokana na hilo sita weza kushirikiana na mtu kwa sababu anauwezo wa kulipa Ada au fedha ya kuwa mwana chama bali nitaangalia shauku iliyo ndani ya mtu katika kufikia hatua kubwa na sito Penda nidanganye kwenye hilo.

Hapa ni vigezo unavyo takiwa kuwa navyo wewe rafiki yangu ili tuweze kufanya kazi pamoja mwaka 2018 ambapo shauku yangu kubwa ni kuona unapiga hatua zaidi kwaka mzima wa 2018,
Karibu sana.

1.Upende kujifunza na Kufanya kwa vitendo,
Mabadiliko ya kweli hayaji kirahisi,Mabadiliko ya kweli yanakuja kwa maumivu makali sana,
Zoezi rahisi kwa kila mtu ni kujifunza/kuongea au kupanga lakini Zoezi gumu na lenye maumivu ni kufanya kwa vitendo au kufanyia kazi yale unayo jifunza na hapo ndio kwenye idadi ndogo ya watu kwa sababu kuna ugumu.

Huwezi kufanikiwa wala kupiga hatua yoyote kwenye maisha kwa kuongea na kupanga pasipo kuchukua hatua au kufanya kwa vitendo.
Hivyo ni lazima ujifunze na ufanyie kazi yale unayo jifunza.

2.Kushirikisha wengine ni Muhimu ili kuhamasika na Kuchukua hatua,
Binadamu tunahamasika zaidi kwa kuona wengine wanamafanikiwa na hivyo ili kuhamasika na kuchukua hatua zaidi ni lazima kushirikishana yale tunayo fanya kila siku au tunayo jifunza katika kufanya mambo mbalimbali kama njia muhimu ya wengine kuhamasika na kuchukua hatua zaidi na kupiga hatua.

Nimekuwa nikishauri watu wengi sana waweze kushirikisha mambo wanayo jifunza na kufanyia kazi na hata uzoefu walio nao kwenye maeneo mbalimbali hii ni kwa sababu inakuwa na msaada mkubwa sana kwa watu wengi kwa kujifunza,kuhamasika na kuchukua hatua zaidi inakuwa inatia nguvu na kuona mambo yanawezekana.

Hivyo ili kuweza kuwepo kwenye programu hii ni muhimu sana wewe rafiki yangu uwe tayari kujifunza kutoka kwa wengine na hata kuwashirikisha wengine kwa ujumla,
Kama ambavyo mimi rafiki yako nitakwenda kuwashirikisha mambo mbalimbali ninayo yaishi kwenye maisha yengu.

3.Shauku ya Kufanikiwa,
Kumpa msaada mtu asie tambua umuhimu wa msaada unao mpa haina maana kwake na kwako pia.

Wapo watu wenye shauku kubwa sana ya kufanikiwa na kila wanapo weka mipango yao mambo huwa tofauti kwa njia hii huyu ndie anaye stahili kupewa msaada wa kufanya nae kazi kwa ukaribu sana ili aweze kufikia hatua kubwa ambayo ana shauku nayo kwenye maisha yake.

Hivyo rafiki ili uweze kunufaika na mpango huu maalumu kwa mwaka 2018 ni lazima uwe na shauku ya kutimiza kitu fulani kwenye maisha yako.

Inaweza kukutisha hii na kuona wewe haustahili kunufaika na programu hii,
Hivyo unaweza kujumuika nami kisha utajifunza na kuhamasika kutokana na hatua za wengine.

4.Ni lazima uwe tayari kuishi misingi muhimu ya mafanikio,
Kutafuta kitu usicho kijua ni adhabu kubwa sana pia kutafuta utajiri na mafanikio makubwa pasipo misingi bado haita kusaidia wewe rafiki yangu kupiga hatua.

Hivyo kama nilivyo kushirikisha kwenye makala zilizo pita kuwa tutakuwa na mambo mengi muhimu ya kujifunza ikiwa ni pamoja na msingi wa maisha ya mafanikio,
Mafanikio yoyote muhimu yanahitaji msingi mkubwa sana na ulio imara kwa sababu pasipo msingi mafanikio hayo yatakuwa ni ya hovyo kwako rafiki yangu.
Karibu tujifunze misingi na kuiishi kwa maisha ya mafanikio makubwa.

5.Mwisho kabisa ni Utayari wa wewe kuwa wewe kwenye maisha yako mwenyewe,
Ghalama kubwa wanazo zitoa watu kwenye maisha zinatokana na wao kuto kuwa wao kwenye baadhi ya maeneo ya maisha yao au kufanya maamuzi ya hovyo kwenye baadhi ya maeneo ya maisha yao kwa kutumia hisia au kuiga wengine wanavyo fanya kwenye maisha yao na hivyo kuendelea kuwa ghalimu na maisha yao kuwa magumu zaidi.

Hivyo rafiki unatakiwa kuwa wewe,Kuwa mwazi ili kuweza kufanya kazi kwa mpango mzuri na mimi rafiki yako.
Tofauti na hapo sito weza kufanya kazi nawe rafiki yangu jambo ambalo sio zuri kimsingi.

Haya rafiki ni machache tu ambayo ni muhimu kuwa nayo hata kabla hujawa na kiwango cha Ada ambayo utatakiwa kulipa ili kuwa mwana chama wa programu hii maalumu.

Karibu sana rafiki yangu ninahakika kubwa utakwenda kupata thamani kubwa zaidi itakao  kuwezesha kupiga hatua zaidi kwa mwaka 2018 na kwenye maisha yako kwa ujumla.
Karibu kupata utaratibu wa wewe kuweza kunufaika na programu hii wasiliana nami moja kwa moja kwa Simu namba WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com.

Karibu sana kwenye programu hii maalumu kwa mwaka huu 2018.

Rafiki/Kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top