Habari rafiki?
Hongera kwa siku hii nzuri sana kwetu ambayo jukumu letu kubwa ni kwenda kuweka juhudi zaidi ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu.
Ni hakika kubwa kwamba unaendelea na mapambano kuhakikisha ushindi mkubwa unakuwa upande wako daima,
Nami na kuongezea neno hapa ENDWLEA KUWEKA JUHUDI kwa sababu juhudi pekee ndio njia ya uhakika ya sisi kuendelea kupiga hatua zaidi na zaidi.
Karibu sana kwenye makala yetu ya leo ambapo leo Mimi rafiki yako nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu linalo wapa watu ushindi wanalo litumia vizuri na wengine kuwa washindwa daima.
Rafiki kushindwa na Kushinda kwako kwenye jambo lolote kunategena jambo moja muhimu sana,
Jambo hili ni MAANDALIZI.
MAANDALIZI,Tofauti ya washindi na watu wanao shindwa ipo kwenye maandalizi,
Kadri unavyo weka maandalizi mazuri ndivyo unavyo zidi kutengeneza nafasi nzuri zaidi ya kufikia mafanikio makubwa.
Iwapo unataka ushindi mkubwa basi unatakiwa kufanya maandalizi makubwa sana na Iwapo utashindwa ujue maandalizi uliyo fanya haya kuwa makubwa kwako ili kukupa ushindi hivyo hutakiwi kufikiri tofauti badala yake rudia upya zoezi la Maandalizi.
Timu moja inapo shinda mchezo maana yake ime fanya maandalizi ya kutosha,
Timu inapo shindwa maana yake inahitaji kuongeza mazoezi zaidi ili kuweza kupanda nafasi hakuna njia ya mkato kwenye hilo kwamba kunanjia ya mkato ya kufikia ushindi pasipo kufanya maandalizi mazuri.
Tofauti ya jeshi linalo shinda vita na lisilo shinda vita ni Maandalizi,
Jeshi lililo fanya maandalizi/mazoezi ya kutosha linakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda vita kwa sababu wakati wa mapigano kila kitu hufanyika kama marudio ya mazoezi waliyo fanya tofauti inakuwa awali walikuwa wanafanya mazozi na wakati huo wanakuwa wapo kwenye mapambano ya moja kwa moja.
Tofauti ya mwalimu anae fundisha wanafunzi na kufaulu vizuri na yule anafundisha na wanafunzi wanashwa mtiani wao Upo kwenye maandalizi ya walimu hao,
Yaani mwalimu anae faulisha anamandalizi makubwa kuliko yule anae felisha.
Tofauti kati ya dreva anae safiri salama na kufikisha abilia salama na wale wanao Pata ajali upo kwenye maandalizi yaani dreva anae fanya safari salama anakuwa na maandalizi mazuri kuliko mwingine.
Iwapo unahitaji kwenda shambani ili uweze kupata matokeo mazuri na yaliyo bora ni lazima ufanye maandalizi mazuri,
Pasipo kuwa na maandalizi hakuna matokeo makubwa.
Hii ndivyo ilivyo hata kwa waandishi na wafundishaji kwenye majukwa mbalimbali ili uweze kufanya shughuli hiyo vizuri na kwa kiwango kikubwa ni lazima uwe na maandalizi mazuri namna ya kuandika na hata namna ya kuwasilisha kwenye jukwaa la moja kwa moja.
Halikadhalika kwenye maisha ya mafanikio ya kila siku,
Watu wote wanao fanikiwa daima wanakuwa na maandalizi makubwa na mazuri zaidi.
Hawa ni watu wanao fanya maandalizi mazuri kabla ya kuanza kufanya jambo wanalo kusudia kufanya na kuwa washindi zaidi.
Siku yako ili iwe na ushindi mkubwa ni muhimu Sana kuwa na maandalizi mazuri sana,
Yaani unatakiwa kupangilia majukumu ya siku yako nzima na muda wake na namna utakavyo weza kufanya kazi hizo.
Utapangilia muda wako kulingana na matukio unayo kwenda kufanya kwa siku husika.
Hivyo rafiki yangu ni muhimu kuwa na maandalizi makubwa kabla hujaamua kufanya jambo lolote ili kuweza kulifanya kwa kiwango kikubwa cha kufanikiwa zaidi,
Huwezi kufanya kwa kiwango kikubwa pasipo kuwa na maandalizi mazuri.
Mfano:Unahitaji kuanza kufuga kuku ni lazima ujue mpango huo utautekelezaje ili uweze kufanya maandalizi ya kutosha,Unahitaji kuwa mshindi kwenye mashindano ya uimbaji labda ni lazima ufanye mazoezi ya sauti na pumzi kama sehemu muhimu ya ushindi wako kwenye jambo hilo,Unahitaji kuandika kitabu ni lazima ufanye maandalizi na kujua kwa kina mahitaji ya kitabu hicho na hata utakavyo tekeleza mpango wako huo.
Hivyo Ushindi wako utaendana kiwango cha maandalizi uliyo fanya,
Vile utakavyo fanya maandalizi mazuri ndivyo utakavyo pata ushindi mkubwa zaidi.
Mwisho kabisa rafiki Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye programu yangu ya Ukocha kwa watu maalumu kwa Mwaka 2018.
Ambapo nitakwenda kufanya kazi na wewe rafiki yangu kwa ukaribu zaidi ambapo nitakufundisha mbinu muhimu kwako katika kukamilisha mikakati yote unayo jiwekea na hata kufikia kwa kiwango kikubwa,Nitakushirikisha mambo mengi kuhusu fedha ambayo ndivyo changamoto kubwa kwenye maisha ya watu wengi kwa nyakati hizi,Nitakushirikisha mambo mengi kuhusu misingi muhimu unayo takiwa kujenga mafanikio yako Nk
Hivyo rafiki unatakiwa kufahamu kwa hakika hayo yote ni mazuri kwako wewe na ili uweze kunufaika na programu hii ni muhimu kwako kuwasiliana nami moja kwa moja ili kuweza kujua utaratibu wake,
Wasiliana nami moja kwa moja kwa Simu namba WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com.
Karibu sana rafiki yangu,
Rafiki/Kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla
Chapisha Maoni