Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio.
Hongera sana rafiki kwa kuendelea kuweka juhudi kubwa katika kujifunza na hata kufanyia kazi yale unayo jifunza kila siku.
Imani yangu kubwa ni kwamba unapiga hatua kubwa kupitia maarifa haya ninayo kushirikisha hapa,
Na iwapo bado hujaanza kufanyia kazi haya unayo jifunza basi haina maana tena kuendelea kujifunza kwa sababu utakuwa unapoteza muda wako bure.
Hivyo hatua kubwa sana baada ya kujifunza ni kufanyia kazi yale unayo jifunza nina kusisitiza kwenye hilo kwa sababu ninayo kushirikisha hapa yote ni yale yanayo ni saidia sana mimi rafiki yako ndio maana nakisisitiza kutumia maarifa haya.
Nichukue nafasi hii ya pekee kukukaribisha kwenye makala yetu pendwa ya leo,
Ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo unalo takiwa kulikwepa kila unapo takiwa kufanya maamuzi yoyote kwenye maisha yako.
Watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baada ya muda kupita na kufikiri kwa undani hujikuta wakifanya maamuzi ya hovyo,
Hii yote ni kwa sababu walifanya maamuzi wakati hawapo kwenye hali ya kawaida.
Jambo hilo ni HISIA watu wote wanao fanya maamuzi yoyote wakiwa katika hisia mbalimbali huwa wanafanya maamuzi yasiyo ya busara,
Mfano;Unapo ahidi kitu ukiwa katika hali ya furaha sana au Kutamka au kufanya kitu ukiwa katika hali ya hasira sana mala nyingi huwezi kufanya maamuzi ya busara hasa unapo kuwa kwenye hali ya hisia hizo mbili.
Unaweza kuahidiwa kitu kwa watu ukiwa katika hali ya furaha sana lakini utakapo kuja kukaa na kutulia kwa undani utakuta hakukua na ulazima wa wewe kuahidi chochote kwa wakati ule,
Au Unaweza kutoa maamuzi au Kutamka jambo lolote ukiwa na hasira unapo tamka au kufanya utaona ni maamuzi mazuri kwa wakati huo lakini jambo hilo hilo Linaweza kuja na sura nyingine hasa unapo pata muda wa kulifikiria kwa kina na muda mwingine jambo hilo unakuta linakuweka matatani hasa linapo fikishwa kwenye maamuzi ya Sheria au utendaji wa haki juu ya jambo hilo.
Ndio maana una shauriwa unapo kuwa na hasira usiongee au kufanya jambo lolote kwa kutumia hisia hiyo,
Kwa sababu madhara ya hisia hiyo ni makubwa mno na yana waghalimu wengi kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao.
Unapo kuwa na furaha ilipo zidi kipimo pia usifanye maamuzi yoyote kwa kutumia hisia hiyo kwa sababu utafanya maamuzi ya hovyo au kufanya maamuzi yaliyo juu ya uwezo wako wewe.
Hivyo rafiki baada ya kuzitambua hisia hizo mbili,
Unatakiwa kutumia Akili ya utulivu na yenye kufanya maamuzi sahihi yaani fanya maamuzi ya u fikiri na sio hisia hii ni kwa sababu maamuzi ya kufikiri yanakuwa ni sahihi zaidi kuliko ya kutumia hisia hizo mbili.
Kwa kutumia ufikiri wako wa utulivu utakuwa umeepuka matatizo mengi sana Pia hii itakuwa ni kinga kwako na kuto kujiingiza kwenye mmatatizo yasiyo ya lazima kwenye maisha yao.
Tumia ufikiri wako wa utulivu kila unapo lazima kufanya maamizi yoyte kwenye maisha yako utakuwa salama zaidi.
Mwisho kabisa nichukue nafasi hii kwenye programu maalumu kwa watu maalumu kwa 2018,
Ambapo nimebakiwa na nafasi chache za watu kuweza kufanya nao kazi moja kwa moja.
Kama nilivyo kushirikisha kwenye maandiko yaliyo pita na kwamba si hitaji idadi kubwa sana ya watu kwa sababu ya ufaanisi wa utekelezaji wa mipango wa wote nitakao fanya nao kazi 2018.
Kupata maelekezo ya kina kuhusu huduma hii wasiliana nami moja kwa moja kupitia mtandao wa Wasapu 0715222989.
Karibu sana rafiki yangu.
Rafiki/Kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla
errynine6@gmail.com
Karibu sana rafiki.
Chapisha Maoni