Habari rafiki na mwanamafanikio kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni tumaini langu kuwa ni mzima na unaendelea vema na shughuli zako za kila siku ambapo unaamini hapo ndipo yalipo mafanikio yako.
Nikukaribishe rafiki kwa moyo mkunjufu kabisa ili tuweze kujifunza pamoja kupitia makala hii ya leo,
Ambapo tutaenda kushirikishana sababu moja inayo wazuia watu wengi kupata matokeo yaliyo bora mala zote wanapo weka juhudi zao.
Na ikiwa ni siku ya kwanza kuingia kwenye mtandao huu basi niku hakikishie juu ya kile utakacho enda kukipata kuwa kitakuwa msaada kwako ikiwa utaamua kuyafanyia kazi yale yote utakayo jifunza.
Rafiki yapo mambo mengi yanayo wazuia watu wengi kupata matokeo mazuri kila wanapo weka juhudi zao kwenye chochote kile,
Lakini sababu iliyo kubwa zaidi ni KUISHIA NJIANI KWA KUKOSA UVUMILOVU NA WOGA WA CHANGAMOTO,
Ni kawaida kwa watu wengi kuwa na woga wa kuchukua hatua na kuanza kufanya chochote kwenye maisha yao,Wengi wamekuwa wakisubili kujazwa hamasa na watu wanao waamini na pindi wanapo hamasika ndipo wanaweza kuchukua hatua.
Lakini wanapo chukua hatua hizo wamekuwa na mtizamo wa aina moja tu,
Mtizamo unao wapa uhakika wa kuwa washindi kwa kila jambo kama walivyo hamasishwa na kuto kuwa na mtizamo wowote juu ya matokeo tofauti na mitzamo yao,
Rafiki ni vizuri kuanza jambo lolote tukiwa na mtizamo wenye ushindi lakini sio mtizamo wenye 100%.
Hivyo kutokana na hali ya kuwepo kwa changamoto nyingi na kukosa uvumilivu katika mitizamo na juhudi zao ndiko kumepekelea watu wengiKUISHIA NJIANI,
Na kuona kama shughuli hizo sio sahihi wao kufanya kwa wakati huo,
Hapa inakuwa ni rahisi kwa mtu kuchukua hatua na kuanzisha jambo lakini anapo kutana na changamoto anakuwa mwoga na anakosa uvumilivu wa kuendelea zaidi badala yake anaishia njiani na hiyo inaonekana kuwa ndio suluu usiyo na maumivu kwao.
Kumbe kuishia njiani ndiko kumewapoteza watu wengi,
Na hata wanapo weka juhudi zao zimekuwa hazina mafanikio kwa sababu hawaja jitoa na kutulia kufanya jambo moja.
Mafanikio ya watu wengi wamezuiwa na tabia ya kuanza jambo na kuacha,
Huku wakianza jambo lingine nalo wanapo kutana na changamoto wanaacha na mwishoni hujikuta wamefanya mambo mengi lakini hawana kitu chochote.
Ikumbuke kuwa mtu anapo anza jambo jipya ana tumia muda mwingi na nguvu nyingi kuliko kuendelea na jambo husika hivyo Ikiwa mtu ataweza kuanza jambo na kushindwa kung'ang'ana nalo ili kupata matokeo hana utofauti na Ndege asie na makazi ya kudumu kwenye kila tawi analo tua au Nyuki akiwa katika kukamilisha majukumu yake ndio anafanya hivyo ili kupata kile anacho kitaka lakini kwetu binadamu ni tofauti tunahitaji kung'ang'ania kusudi letu katika kufanya kila jambo.
Kuishia njiani ndiyo ugonjwa unao waadhiri wengi kwenye nyanja mbalimbali za mafanikio yao,
Imekuwa ni rahisi kuanza kuliko kuendelea na safari kumbe shida kubwa ipo kwenye kuanza na unapo kuwa na mwanzo mzuri kuendelea ni rahisi hata kama kitu unacho fanya kinachangamoto nyingi sana.
Mwisho kabisa ni hitimishe kwa kusema hivi,
Rafiki hatua unayo takiwa kuifuata sasa ni kuanza kufanya chochote kwa ubora na Kukimaliza usiishie njiani mpaka pale utakapo pata hitaji lililo kufanya ufanye hicho.
Unatakiwa kufahamu kuwa hakuna urahisi wa mafanikio zaidi ya kukomaa na kung'ang'ana na kutafuta matokeo unayo yataka ukiwa na mtizamo chanya zaidi maana sio rahisi.
Na ikiwa utakosa uvumilivu wa kupambana na changamoto basi ujue huto fikia kusudi lako la kufanya hicho,
Yaani hapo ulipo ni mahali sahihi kwako kuwepo sasa ila unacho hitaji ni kuwa na uvumilivu wa kupambana na changamoto na kuhakikisha unazishinda kwa namna yoyote ile.
Kila la kheri rafiki yangu,
Ninahakika utaenda kuyafanyia kazi haya machache niliyo kushirikisha leo na ninaimani yatakupa matokeo makubwa sana na yaliyo bora zaidi.
Na wako Mwandishi|Mjasiriamali & Mwamasishaji
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni