Unknown Unknown Author
Title: Soma Hapa Tabia Moja Unayo Paswa Kuwa Nayo Makini Kwenye Biashara Yako.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio, Ni imani yangu kuwa unaendelea vema na majukumu yako...

Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kuwa unaendelea vema na majukumu yako ya kila siku ambapo ndilo chaguo lako lilipo na unafanya kwa ubora na utofauti mkubwa kuliko yeyote.

Pia hongera kwa siku hii muhimu zaidi ambapo unaamini juhudi zako sio bure ni lazima zizae mafanikio unayo yataka.
Karibu rafiki tushirikishane tabia iliyo sumu kubwa kwa biashara na hivyo kutokana na uwepo wa chembe ya tabia hii biashara nyingi zimekuwa zikifa,
Hivyo rafiki nakwenda kukushirikisha tabia hii na kukupa njia pekee itakayo kujengea biashara yako kuwa na wateja wanao ithamini biashara yako.

Rafiki zipo tabia nyingi sana zinazo weza kuiua biashara yako na kuto kuwa na wanunuzi au watumiaji wa bidhaa au huduma yako,
Lakini kwa siku hii ya leo nitakushirikisha moja na hata namna ya kuikwepa tabia hii.

Tabia hii ni UONGO/UDANGANYIFU,
Siku hii ya leo nitakwenda kukushirikisha sumu ya wongo inavo ua biashara nyingi kubwa kwa ndogo.

Uongo na Uaminifu ni tabia ambazo kila mmoja anaweza kujijengea katika maisha yake na kuziishi kama sehemu kubwa ya msingi wa maisha yake,
Na hivyo kutokana na tabia hii mtu kila anacho fanya anahakikisha kinasimamia kwenye Ukweli na Uaminifu iwe ni katika shughuli za kibiashara na hata sehemu zingine za maisha yake.

Na ikiwa mtu ataweza kujijengea tabia hii nakuishi kama sehemu ya maisha yake ni wazi kuwa ameamua kuishi uhalisia wake,
Kutokana na kuishi uhalisia wake  anakuwa tayari anajitengenezea nafasi kubwa kwa kila anae mzunguka.

Turudi kwenye somo letu la leo,
Swala la wongo linakuwa pale mtu anapo ishi maisha ambayo hana uwezo nayo,
Mtu hana uwezo na jambo fulani lakini analazimisha alifanywe kwa nguvu na linapo onyesha kumshinda atalazimika kudanganya ili apate mda zaidi wa kulikamilisha jambo hilo,
Tabia hii ya Uwongo/Udanganyifu ndiyo inayo ua biashara nyingi na kwa kasi kubwa hii ni kutokana na wanunuzi au watumiaji wa huduma husika kukerwa na tabia hiyo.

Wafanyabiashara/Watoa huduma wengi ni wadanganifu,
Wengi hawaishi uhalisia wao jambo ambalo linapelekea huduma zao kukosa wateja wa uhakika na kuwa na wasiwasi juu ya upatikanaji wa huduma wanazo hitaji.
Mfano:Mimi ni dobi mteja amefata huduma lakini simhudumi kwa wakati na hata ninapo mpa mda wa kuipata huduma yake ninamdanganya anapo kuja inakuwa bado,
Mfano mwingine Ni pale unapo mwahidi mteja wako njoo mda fulani utaikuta huduma unayo hitaji na mteja anapo kuja anatoa sababu nyingi zisizo kuwa na ukweli wowote kwa mteja,
Mtu anauza bidhaa anajua kabisa bidhaa hiyo hana na anamruhusu mteja wake kuilipia bidhaa hiyo na unapo fika muda wa kumtumia bidhaa anaanza sababu ambazo mala nyingi huwa ni kero kubwa kwa mteja wake,

Kutokana na uwepo watabia kama hizo hapo juu au zingine zinazo fanana na hizo ni wazi biashara yako inaweza kufa kwa kukosa wanunuzi au watumiaji wa huduma yako hata ungekuwa ni bidhaa zenye ubora kiasi gani.
Na hata inapo tokea unawateja wanao weza kuivumilia biashara yako bado wanakuwa hawakuamini kwa namna yoyote na mala zote ufanyaji wa biashara hiyo unakuwa mgumu sana.

Rafiki kama wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia kama hizo Unatakiwa kubadilika na kujijengea tabia itakayo kupa watu sahihi kwenye biashara yako,
Watu watakao kuamini wewe na biashara yako pia.
Usipo weza kufanya hivyo basi huwezi kuwa na watumiaji wa huduma yako na kwa mfumo wa kukosa wa tumiaji wa huduma yako ni lazima itakufa maana hakuna huduma inayo weza kuishi pasipo wateja/Mauzo.

Kumbuka Uaminifu licha ya kuwa ni tabia  itakayo kupa watu sahihi kwenye biashara ni Mtaji mkubwa kwa maana hiyo hata inapo tokea umeyumba ni rahisi kupata msaada kutoka kwa watu wanao kuamini kwenye biashara yako.

Uongo/Udanganyifu ni sumu kubwa inayo ua biashara za watu wengi,
Hivyo kama utashindwa kuishi ukweli na uhalisia wa maisha yako ya sasa basi huwezi kupata watu sahihi kwenye huduma yako.

Mwisho kabisa ni malize kwa kusema Uaminifu unalipa kwenye kila kitu,
Hivyo kama ukishindwa kujijengea tabia ya Uaminifu sawa na kuchagua kukosa vingi kwenye maisha yako,
Hauto weza kuwa na watu sahihi watakao kuamini wewe na hata biashara yako.
Uaminifu unalipa sana na hivyo anza kujijengea tabia ya kuwa mwaminifu kwenye kila unacho fanya.

Kila la kheri rafiki yangu,Nikutakie siku njema na yenye mafanikio.
Na  Mwandishi /Mjasiriamali & Mwamasishaji

Ernest Lwilla

Pia unaweza kutuma ujumbe kwenye mamba hii WhatsApp 0715222989 uunganishwe na kundi la WhatsApp BURE.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top