Unknown Unknown Author
Title: Hii Ndiyo Sehemu Pekee Unayo Weza Kuchukulia Mkopo Wako
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu, Nitumaini langu u mzima wa afya njema kabisa. Ikiwa ni siku nyingine iliyo yapekee zaidi kwetu ...

Habari rafiki na mwanamafanikio mwenzangu,
Nitumaini langu u mzima wa afya njema kabisa.

Ikiwa ni siku nyingine iliyo yapekee zaidi kwetu zaidi tukiendelea kufanya kazi kwa juhudi na kwa kujituma ili kupata matokeo makubwa zaidi na yaliyo bora zaidi.
Karibu tena rafiki mpendwa msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo wa mafanikio.

Rafiki siku hii ya leo nimeamua kukushirikisha Sehemu moja muhimu unayo weza kuchulia mkopo popote ikiwa utakuwa na ulazima,
Nianze kwa kusema Huwezi kununua nguo za jinsia yoyote Eti kwasababu unaujauzito,
Nilazima Ujifungue na Ujue jinsia ya mtoto ndipo ununue nguo.

Kwanini nasema hivyo??
Ni kwa sababu watu wengi wanajipoteza kwenye maeneo waliyo chagua kuwa bora kwa sababu ya kukosa subila ya kuona ni jinsi gani mawazo yao yatakuwa na matokeo chanya.
Watu wengi wanajiingiza kwenye matatizo ya kudaiwa kwa kigezo cha kuwa na wazo wanalo amini litakuwa na matokeo mazuri,
Kupatikana kwa wazo linalo onekana kuwa bora kwao imekuwa ni sababu ya kuchukua hatua ya kukopa jambo ambalo sio sawa kabisa.

Rafiki hii nimeona kukuweka wazi na kwamba hupaswi kukopa kwa sababu una wazo bora na unalo liamini kibiashara,
Hutakiwi kukopa kwa sababu wengine wana fanya hivyo,Hutakiwa kukopa kwa sababu umeaminishwa biashara unayo ainza inalipa,
Zaidi kabla hujapata wazo la kukopa ni lazima ujiulize wazo hilo linaghalimu kiasi gani na kujipa muda wa kukusanya kianzio cha kukuwezesha kulifanyia kazi wazo lako,
Jipe muda ukiwa katika hatua muhimu za kupata taarifa za biashara husika ndio muda wa kujiandaa kidogo kidogo nakuhakikishia rafiki huto chelewa chochote zaidi utakuwa umejiweka salama.

UNAHITAJI KUWA NA NINI ILI UKOPE??
Rafiki kama nilivyo weza kukusisitiza hapo juu hutakiwi kukopea wazo la biashara,
Badala yake KOPA MKOPO WA BIASHARA UNAYO IFANYA,
Naomba unielewe vizuri hapo rafiki yangu.
Unahitaji kuwa na biashara ambayo unauzoefu nayo kwa kipindi kisicho pungua mwaka mmoja hapo ndipo unaweza kukopa kama kutakuwa na ulazima wa biashara yako kukopa.

Biashara inayo hitaji mkopo sio ile ambayo imefilisika au biashara iliyo punguza mauzo kwa sababu ambazo sio za kimtaji,
Pia Unapo chukua hatua ya kukopa hakikisha biashara yako mtaji wake ni mkubwa zaidi ya mkopo wako na kama mkopo utakuwa mkubwa zaidi ya mtaji wako basi hakikisha unavitega uchumi vitakavyo kusaidia kuulipa mkopo wako hata zinapo tokea changamoto za kushuka kwa mauzo ya biashara uliyo kopea.

Zingatia hili unapo hitaji mkopo wako,
Usichukue mkopo kama unaanza biashara mpya kwa sababu zipo changamoto nyingi kwenye maeneo mbalimbali ya kuanzisha  biashara mpya,
Usichukue mkopo mkubwa kuliko mtaji uliopo kwenye biashara yako Mfano:Mtaji uliopo kwenye biashara yako ni Mil 10,Basi hutakiwi uchukue mkopo Mil 15 badala yake nakushauri mkopo uwe mdogo kuliko mtaji wako,
Usiweke kiasi chote cha mkopo  kwenye biashara.
Nina kushauri chukua tahadhari  kwa hatari na changamoto zozote zinazo weza kukukwamisha wakati wa kurejesha mkopo wako.

Mwisho kabisa,
Sikwambii kwamba mikopo ya biashara ni mibaya hapana Bali Mikopo ya mahitaji ya maisha ni mibaya zaidi,
Usikope pasipo kuwa na sababu ya kukopa na usikope kwa sababu ya mahitaji yasiyo husiana na uzalishaji zaidi.

Kumbuka wapo watu wanao piga hatua kubwa zaidi kwenye mafanikio yao ya kimaisha kupitia mikopo,
Na kuna watu wanao uziwa mali zao na hata  kufilisiwa kwa biashara zao kwa sababu ya mikopo hasa watu wanao kopa kwa ajili ya kukamilisha mahitaji yao Mfano:Mtu anakopa ili kununua gari la kutembelea au Mtu anakopa kwa mahitaji ya malezi ya familia na hana mfumo mzuri wa uzalishaji ili kuweza kurejesha mkopo huo.

Rafiki hakikisha mkopo wako unazalisha na unajirejesha wenyewe,
Yaani mkopo uwe ni wakuzalisha na uweze kujirejesha wenyewe na sio wewe.

Tuma ujumbe mfupi BIG KEY OF SUCCESSFULLY2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gamili.com
Uunganishwa na group la WhatsApp BURE.

Kila la kheri rafiki yangu na msomaji wa makala zetu,
Ni wako rafiki katika mafanikio yako.

Ernest Lwilla

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top