Unknown Unknown Author
Title: Mambo 2 Muhimu Unayo Takiwa Kufanya Kabla Huja Nunua Chochote.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari ya leo mpendwa msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa UFUNGUO WA MAFANIKIO, Ni tumaini langu unaendelea kuyafanyia kazi yale...

Habari ya leo mpendwa msomaji wa makala zetu kupitia mtandao huu wa UFUNGUO WA MAFANIKIO,
Ni tumaini langu unaendelea kuyafanyia kazi yale yote unayo jifunza hapa na hiyo ndiyo sababu kubwa ya wewe kuendelea kujifunza zaidi.

Karibu rafiki niweze kukushirikisha jambo kubwa linalo wasumbua watu wengi hasa linapo kuja swala la fedha ipo mkononi lakini Afanye nini ili fedha yake asiipoteze pasipo jambo la msingi.
Hili lipo kwa wengi hujikuta wamenunua bidhaa ambayo haina umuhimu wowote kwao ila wamesha,
Bila shaka ulisha wa kununua kitu ambacho tangu ulipo nunua umekitumia mala moja tu na huna haja ya kukitumia tena.
Bila shaka ulisha wai kusafiri na ukiwa safarini ukanunua kitu ambacho hukuwa na mpango wewe ila kwa ushawishi wa wauzaji ukajikuta unapewa umuhimu wa bidhaa au kuona kama bidhaa hiyo unaipata kwa bei rahisi na hivyo usipo ipata hapo huto ipata tena.

Rafiki kwanza awali ya yote unatakiwa kufahamu yeyote unae mwona na bidhaa popote shida yake kubwa ni kuuza lakini hajui nani atamuuzia hivyo anapo kuona wewe anatumia kila mbinu kukushawishi ili aweze kuuza bidhaa yake,
Hapo anatumia kila mbinu itakayo wezekana ili asirudi na bidhaa yako,
Tuachane na hayo yote turudi kwenye jambo letu la msingi ninalo hitaji kukushirikisha leo hii.

Rafiki mtu pekee mwenye maamuzi na fedha yako ni wewe,
Wewe ndiye unaye panga pesa yako ifanye nini na sio pesa yako ndiyo ikupangie cha kufanya hivyo kwa kutambua uhalali wa umiliki wa pesa yako unao uwezo wa kupanga mambo muhimu ambayo pesa yako itakufanyia.

Jambo la kwanza TOKA NA BAJETI YAKO NYUMBANI,
Jambo kubwa unalo hitaji kufanya ni kuaanda bajeti yako ya siku nzia au ya manunuzi yako na kama unajua bei ya bidhaa unazo hitaji piga kabisa na jumla ya ghalama na hiyo ghalama ndiyo uondoke nayo nyumbani.
Ukiwa katika manunuzi yako hutakiwi kununua chochote ambacho hakipo kwenye orodha ya bidhaa ulizo panga kununua,
Ukiwa katika manunuzi hayo unaweza kutengeneza orodha nyingine ya bidhaa unazo ziona na kisha kurudi nayo nyumbani kwa upembuzi zaidi ya mahitaji hayo.

Rafiki ni nguo ngapi ulisha zinunua na kuvaa mala moja na hukuwai kuvaa tena??
Unadhani kwanini imekuwa hivyo??
Ni kwasababu ulinunua kwa kushawishiwa na haikuwa kweje bajeti yako,
Ulinunua kwa sababu umepewa faida zake lakini hukuwa na uhitaji wa nguo hiyo,
Hivyo unatakiwa kupanga bajeti yako na sio kupangiwa na waazaji.

Jambo la pili ANDIKA FAIDA NA HASARA 5 ZA BIDHAA UNAYO TAKA KUNUNUA,
Ili uweze kununua vitu muhimu kwako na vinavyo hitajika huku ukiwa umeepuka kabisa vishawishi vya wauzaji wa mitaani,
Nilazima uwe na orodha ya mahitaji utakayo yanunua na kujua kila hitaji linahitajika kwa kiasi gani??
Je ni hasara zipi zitatokea kama utaikosa bidhaa hiyo??
Kwa kutambua mambo matano ya faida na mambo matano ya hasara ikiwa utaikosa bidha husika huwezi kununua bidhaa pasipo kufanya hivyo,
Pia kwa kufanya hivyo tu utajikuta kila unacho nunua kina kuwa na matumizi zaidi ya moja na hivyo unaweza kuwa na vyombo vichache vinavyo kukamilisha mahitaji yako yote.

Je unafanya nini unapo kutana na bidhaa inayo onyesha kuwa na umuhimu kwako na ghalama yeke ni ndogo kwa wakati huo??

Unacho takiwa kufanya ni hiki kurudi na wazo na kuliweka kwenye mchakato wako wa kujua faida tano na hasara za bidhaa hiyo kwako.
Kama haitoshi weka kwenye orodha ya mahitaji muhimu ambayo utatakiwa kufanyia manunuzi pindi utakapo panga wewe na sio vishawishi wa wauzaji,
Ambao mida wote wanafikiri kuuza tu kwa namna yoyote ile ni lazima wafanye ushawishi wakuhakikisha wanauza tu.

Je ufanye nini Unapo pungukiwa au kuzidi kwa fedha wakati wa manunuzi yako??

Ukweli muda mwingine unaweza kuwa na orodha ya bidha lakini orodha hiyo isiwe na ghalama sahihi za bidhaa husika inaweza kupungua au kuongezeka,
Hivyo ikiwa bajeti itaongezeka unacho hitaji ni kununua mahitaji ambayo yata endana na fedha yako tu na mahitaji yatakayo baki weka alama ya kosa na kuyaingiza kwenye bajeti itakayo fuata.
Pia bajeti inapo kuwa ndogo na hivyo pesa kubaki,
Usinunue chochote ambacho hakipo kwenye orodha yako ya manunuzi.

Hata inapo tokea bajeti yako kuwa ndogo usikope mahitaji hayo maana hali hiyo inakuwa tayari imekubadilishia mfumo na kuingia kwenye madeni ambayo wewe hukuyategemea na wala sio mihimu kwako.

Mwisho kabisa nikutakie kila la kheri kwenye matumizi mazuri ya kila fedha itakayo ingia mkononi mwako,
Hakikisha inafanya yale yote yaliyopo kwenye orodha yako wewe maana wewe ndiye unae paswa kuiendesha pesa na sio pesa kukuendesha wewe kwa namna yoyote.
Tumeumbwa kutawala na sio kutawaliwa na hali ya hisia za mazingira tuliyopo.

Rafiki nikutakie utekelezaji wa dhati na matokeo mazuri kwako.

Tuma Ujumbe BIG KEY OF SUCCESSFULLY2017 kwenda 0715222989/Email.errynine6@gmail.com
Uunganishwe na group la WhatsApp
BURE.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top