Habari rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio?
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na unaendelea vema na mapambano ili kuendelea kutengeneza nafasi ya wewe kufikia mafanikio makubwa zaidi.
Jambo pekee unalo takiwa kulifahamu kwa kina ni kwamba kila unapo weka juhudi zaidi ndivyo vikwazo vinavyo kuwa vingi zaidi,
Hivyo Dawa pekee ya wewe kuendelea kuwa mshindi kila siku ni wewe kuto kukata tamaa.
Nichukue nafasi ya pekee kukukaribusha kwenye makala yetu ye
a leo ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu ambapo unatakiwa kuliishi na kulifanyia kazi kwenye kila hatua ya maisha yako na iwapo utaacha kulifanya jambo hilo basi utakuwa umesha anza kuweka juhudi za kurudi nyuma na sio kwenda mbele tena.
Rafiki watu wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao malabaada ya muda mfupi toka wanapo kuwa wanaanza kufanya jambo hayo kwenye maisha yao,
Kama ambavyo unajua mtu anapo anza biashara mala nyingi huwa anaweka juhudi kubwa sana katika kufanya jambo hilo,Kujifunza na kufanya maboresho kila siku hasa kutokana na matokeo ambayo anakuwa anapata na hivyo iwapo matokeo anayo pata hayakuwa tegemeo lake basi anakuwa na njia ya kubadili jambo hilo.
Lakini Anapo kuwa amefikia hatua ambayo kama ni biashara imesha anza kuzalisha faida kubwa basi analizika na kuacha kufanya mambo hayo kwenye maisha yake na hapo ndio mwanzo wa watu wengi kuto piga hatua na wengine hupelekea kuishia hapo hapo.
Rafiki jambo hili ni KUJIFUNZA KILA SIKU,
Watu wengi wanapo Anza kufanyia kazi mawazo yao huwa ni watu makini sana wanao taka kujua kila kinacho endelea kwenye yale mambo muhimu wanayo kuwa wanafanya,
Hatua hii ya kuwa karibu na kufatilia kwa undani huwa ni ngazi kubwa sana yao katika kupiga hatua zaidi katika kusonga mbele hatimae kufikia katika hatua kubwa ya mafanikio.
Watu hawa huwa ni wadadisi,Huwa ni wafuatiliaji wa kila kitu wanacho kifanya,Huwa ni watu wa kujifunza kila muda na kila siku na hata kuwa ni watu wa maamuzi sahihi hasa pindi wanapo takiwa kufanya marekebisho muhimu kutokana na matokeo wanayo kuwa wanapata kwenye hatua hizo muhimu za maisha yao.
Lakini pamoja na kuweka juhudi hizo kubwa siku za awali bado hufikia hatua huanza kufanya mambo kwa mazoea hasa wanapo kuwa tayari wamesha yazoea mambo hayo,
Wanakuwa hawaoni tena nafasi ya kujifunza wala kufanyia maboresho ya yale muhimu wanayo jifunza.
Mtu anapo fikia hatua hii ya kuona hakuna sababu ya kujifunza tena basi hiyo inakuwa ndio tiketi ya wao kuanza kurudi nyuma au kubaki pale pale bila kupiga hatua yoyote kwenye maisha yao.
Rafiki jambo pekee unalo takiwa kulifahamu na kuwa makini nalo siku zote za maisha yako ni kwamba Maisha ndio chuo pekee kisicho na kikomo wala kuishiwa mambo ya kujifunza,
Yaani iwapo unaishi basi hiyo ni fursa ya kujifunza mpaka mwisho wa uhai wako,Unapo ingia kwenye kazi yoyote au biashara yoyote basi unakuwa ndio umejiandikisha kwenye chuo chenye masomo mengi na yasiyo na kikomo lakini Unao uhuru wa kuchagua kipi ujifunze na kipi usijifunze.
Rafiki unapo ona umesha fikia hatua ya kukifahamu kitu kwa undani na kuona hakuna nafasi ya kujifunza tena basi ujue huo ndio mwisho wako kufanya kitu hicho kwa mafanikio,
Hii ni kwa sababu maisha kila siku yanabadilika,Biashara kila siku zinabadilika,Kazi kila siku zinabadilika,Dunia na mambo yote yanabadilika sasa utakapo fikia hatua ya kuishi bila kujigunza mabadiliko yanayo tokea basi ujue ndio mwisho wako.
Hivyo rafiki Unatakiwa kuweka juhudi kila siku kwenye kila eneo la maisha yako,
Weka juhudi ya kujifunza na kufanyia kazi yale unayo jifunza,Weka juhudi kubwa ya kwemdana na mabadiliko ambayo kila siku yana tokea kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako na hata jamii inayo kuzunguka kwa kufanya hivyo utakuwa na uhakika mkubwa wa kuendelea kusonga mbele na kuona fursa nyingi kwenye kila mabadiliko yanayo tokea.
Mwisho kabisa rafiki kazana sana kujifunza kila siku,
Unapo fikia hatua ya kuishiwa maarifa basi ujue ndio mwisho wako kupiga hatua hii ni kwa sababu maarifa yanakuwa na kuongezeka kila siku na kukua na kuongezeka huko ndiko kunakupa mafanikio wewe hasa unapo fanyia kazi yale Unayo jifunza.
Nichukue nafasi hii pia kukukaribisha kwenye programu maalumu kwa watu maalumu 2018,
Ambapo tukiba bado mwanzoni mwamwaka nimetoa nafasi chache sana kwa watu wanao Penda kujifunza na kufanyika kazi yale wanayo jifunza kila siku kuweza kuwashika mkono zaidi kwa kuwapa maarifa zaidi ambayo yatawasaidia kufikia malengo yao kwa mwaka 2018.
Zaidi nitakuwa karibu kwa kila hatua kwenye chochote unacho fanya na hatua unazo piga kila siku.
Karibu sana tufanya kazi kwa pamoja ambapo nitakwenda kufundisha na kushauriana zaidi na kwa ukaribu sana.
Karibu sana rafiki yangu,
Na wako rafiki katika mafanikio
Wasiliana nami kupitia What'App namba na email zilizopo hapa chini.
Rafiki/Kocha & Mshauri wako
Ernest Lwilla
0715222989/errynine6@gmail.com
Karibu sana rafiki.
2018 Kuwa Bora Zaidi.
Chapisha Maoni