Habari rafiki na msomaji wa maandiko yetu kupitia mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa kuwa ni mzima wa afya njema na unaendelea vema na shughuli zako za kila siku na hiyo ndio njia ya uhakika kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa sana.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu sana unalo takiwa kuliepuka kwenye maisha yako ili usiweze kuingia au kuingizwa kwenye matatizo na watu wengine kama ambavyo wengi wamejikuta kwenye matatizo bila wao kujua ni kwa namna gani wameingia au kuingizwa.
Watu wengi hawa pendi kuingia kwenye changamoto ya aina hii lakini katika nyakati ambazo wao wenyewe hawajitambui basi wanajikuta kwenye dimbwi hilo na baadae kuwa kero kwao,
Jambo hili rafiki ni WATU KUAHIDI VITU VILIVYO NJE YA UWEZO WAO.
Kunahali fulani hutokea kwenye nyakati za watu kuahidi hasa wanapo pewa nafasi ya kuahidi na hivyo katika kuitumia nafasi hiyo hufanya kosa kubwa la kuanza kutizama wengine wame ahadi nini? Kisha kuona wao wataahidi nini?
Kwenye hatua hiyo pia mtu anajihoji Je ni ahidi kipi kitakacho kuwa na hadhi kwenye kundi zima?
Hapo ndio chanzo cha matatizo yote huanzia na wengi kujikuta kwenye matatizo.
Unapo ahidi kitu ambacho kwa muda huo hauna tayari umesha jiingiza kwenye matatizo,
Unapo ahidi kitu ambacho hakipo mfukoni mwako tayari umesha jiandikisha DENI kwa namna yoyote utalazimika kudaiwa na hata kulilipa.
Tatizo hili kwa wengi hutokana na kuto kuwa wakweli kwa wao wenyewe,Watu kuishi kitu ambacho kila mtu anaishi na hata kuahidi kwa sababu wamepewa nafasi ya kufanya hivyo,
Ni uamzi wa hovyo sana hata kama unauhakika wa kutekeleza ahadi hiyo usiahidi kwa sababu kesho huijui na hata kama unaijua bado huna uhakika mkubwa wa ktekeleza ahadi yako.
Changamoto kubwa ni kwa watu ambao umewaahidi ni kwamba ahadi yako inaingizwa moja kwa moja kwenye bajeti na hivyo inapo tokea hujatekeleza ahadi hiyo tayari inakuwa wewe ndio mbaya kwa sababu umekwamisha zoezi hilo kufanyika.
Matatizo ya kuahidi hutokea zaidi wakato fulani mtu anapo kuwa kwenye hali isiyo ya kawaida hali ambayo kwa kiwango kikubwa inakuwa imetawaliwa na hisia Mfano:Hasira,Furaha sana na hata maumivu,
Hapa ndipo watu hufanya maamuzi ya hovyo ya kuahidi mambo mengi yaliyo nje ya uwezo wao.
Mfano:Upo kwenye sherehe ya harusi ukasimamishwa mbele za watu na kuambiwa utoe zawadi alafu unakuwa hukufanya maandalizi yoyote hapa watu wengi hutoa maamuzi ya sio ya busara na yasiyo pewa nafasi ya kufikiriwa hata mala moja,
Yaani mtu anaahidi kitu ambacho hata hakupanga na baada ya muda au siku moja au mbili hapo ndipo akili inakuwa imetulia ndipo anapata nafasi ya kufikiri hapo ahadi hiyo mala nyingi inageuka kuwa pasua kichwa kwa mtu huyo.
Lakini pia ahadi zinazo tolewa wakati watu wana hasira,
Mfano:Wakati wa ukusanyaji wa fedha ya kufanya jambo fulani hapa wengi hujikuta kwenye fileni ya kupigiwa simu kila muda na hivyo ili kuzima wasipigiwe simu basi wanalazimika kuahidi na muda unapo fika anaanza kujihoji iv niliahidi leo?
Hii ina kuonyesha ni kwa namna gani ahadi hiyo haikupewa muda wa kufikiliwa hata kidogo akilini kwa mtu huyo.
Rafiki usiahidi kitu kilicho nje ya uwezo wako kwa muda huo hata kama unauhakika fedha hiyo kuna mahali ipo,
Unapo pewa nafasi ya kuahidi usifanye hivyo badala yake toa kiwango ulicho nacho kwa wakati huo.
Unapo pewa nafasi hiyo nawe kufanya hivyo Unakuwa tayari umesha ingia kwenye mtego wa kudaiwa.
Sasa nimesha andika mengi huko nyuma kuhusu kudaiwa na madhara yake lakini kubwa zaidi ni kwamba utakosa utulivu wa kufanya kitu unacho kifanya.
Mwisho kabisa nafasi za kuahidi uwa zinatolewa kwenye maeneo yaliyo jaa hisaia kubwa ili kuhakikisha wengi wanaahidi na kwa njia hiyo wanakuwa na watu wengi wanao ahidi na mtu akisha ahidi inakuwa uhakika kwa watu hao kupata fedha.
Na mbaya zaidi hapa wengi hushindwa kabisa kutumia maneno yenye machungu na yenye kuwaangusha watu maneno kama Sina fedha,Hapana,Sito toa n.k
Hivyo nenda ukawe wa tifauti kabisa kwa kuto ahidi kitu kilicho nje ya uwezo wako kwa wakati huo,
Usiahidi toa fedha iliyopo kwa wakati huo,Ukiahidi umejiingiza kwenye matatizo makubwa sana.
Unapo tumia nafasi ya kuahidi tayari unakuwa umetumia nafasi hiyo kujiandisha kudaiwa.
Kila la kheri rafiki yangu,
Nichukue nafasi hii pia kukukaribisha kwenye Programu maalumu kwa watu maalumu 2018,
Ambapo kwa sasa zimebaki nafasi chache sana za wewe rafiki yangu kupata couching na kusimamiwa na mimi rafiki yako moja kwa moja na kufanya kazi kwa pamoja.
Karibu sana kwenye kundi la THE DOLD MIND tuweze kujifunza na hata kujadiliana pamoja kwa kina.
Iwapo utachukua hatua hiyo ni wazi utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kupata kitabu changu litakapo kuwa tayari muda wowote.
Kupata maelezo zaidi wasiliana nami moja kwa moja kwa namba 0715222989 WhatsApp/errynine6@gmail.com
Rafiki,Kocha&Mshauri wako
Ernest Lwilla.
Chapisha Maoni