Unknown Unknown Author
Title: Hiki Ndio Kitu Kinacho Tafutwa Na Watu Wasio Na Mafanikio Kutoka Kwa Walio Fanikiwa.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Alikili Yako Inakijua kitu hiki ila huja amua kuchukua hatua(Hakuna siri na Kama kuna siri basi unaijua). Habari rafiki na mfuatiliaji wa m...

Alikili Yako Inakijua kitu hiki ila huja amua kuchukua hatua(Hakuna siri na Kama kuna siri basi unaijua).

Habari rafiki na mfuatiliaji wa mtandao huu wa Ufunguo Wa Mafanikio,
Ni imani yangu kubwa unaendelea vizuri na mapambano ili kuendelea kujitengenezea nafasi kubwa ya wewe kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako kuelekea mafanikio yako.

Karibu sana rafiki kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu sana ambalo limekuwa kikwazo kwa watu wengi kuchukua hatua huku wakijipa imani na kwamba labda wakikijua kitu hicho basi itakuwa ni njia rahisi kwao kupiga hatua.

Nianze kwa kusema HAKUNA USICHO KIJUA,
Watu wengi wanatafuta kuijua  siri kuu inayo watofautisha watu wanao fanikiwa sana na wale wasio fanikiwa na kwa bahati mbaya sana wakati watu wasio fanikiwa wanakazana kutafuta kitu hicho ndivyo wanavyo fanikiwa wanavyo zidi kufanikiwa zaidi kila kukicha.

Kitu hiki ni SIRI YA MAFANIKIO Wenda na wewe rafiki yangu ulisha wai kujiuliza au kujipa majibu rahisi kwamba kuna siri inayo wapa watu mafanikio makubwa na wengine kuto fikia mafanikio hayo.

Kwanzia leo wewe rafiki yangu ondoa dhana hiyo ya kwamba kuna siri ya mafanikio na jua kuwa hakuna siri ya mafanikio kwa watu wanao fanikiwa ila kunamisingi wanayo ifuata na kuifanyia kazi ndio maana wanafanikiwa zaidi,
Misingi hiyo na wewe unaigahamu sana tena kwa namna ya pekee sana lakini unaipuuza sasa kwa kuipuuza misingi hiyo ndivyo unakuwa kwenye hali mbaya zaidi kiasi kwamba unakuwa unahisi kuna uchawi ulio kizuizi kwako kufanikiwa zaidi.

Labda nikuulize rafiki yangu ni mala ngapi umelisikia Neno AKIBA?
Je wewe unaliishije kwenye maisha yako?

Je ni mala ngapi umelisikia neno Uwekezaji?
Wewe unaliishije neno hilo?

Je ni mala ngapi umesikia Neno Ubahili?
Je wewe unaliishije?
Kwanini wengine wanaitwa bahili wakati huo wewe unaonekana kuwa ni mtu mwenye pesa nyingi sana kwa nje na ndani unakuwa na changamoto kubwa za uchumi na kifedha?

Mpaka hapo rafiki yangu umesha anza kupata picha kamili kwamba hakuna siri inayo wapa watu mafanikio lakini kunamisingi inayo wapa watu mafanikio,
Misingi hiyo kwako sio migeni No! Unaifahamu sana lakini hufanyii kazi misingi hiyo.

Nimesha andika makala nyingi huko nyuma namna bora unayo weza kutenga na kuweka fedha ya akiba,
Nimesha kushirikisha njia bora ya kuweka akiba yako hata kama kipato chako ni chini ya Tsh 1000 na mwishoni kabisa nikakushirikisha na kanuni kuu ninayo Iishi mimi (Kama nimekula basi nimesha weka akiba).

Wewe rafiki yangu kuendelea kufikiri kuwa kuna siri ya mafanikio ni kupoteza muda wako na nguvu zako kwa sababu muda utaisha ukiwa bado hauna siri huku matajiri wakizidi kuwa matajiri zaidi.

Msingi mwingine Muhimu zaidi ambao watu wenye mafanikio makubwa huishi ni Kuwa na matumizi madogo kuliko mapato yao,Sasa kwa watu wanao tafuta siri ya mafanikio kuishi msingi huo ni sawa na kujitesa na hapo ndipo hutumia fedha zote wanazo pata bila kuifikiria kesho na hapa wengi utawasikia kesho itajisumbukia yenyewe jambo ambalo ni hatari zaidi hasa ukiangalia kuwa muda haukungoji wewe.

Ukiwa katika hatua za kutafuta siri hapo unajikuta kwenye matatizo zaidi na kujikuta kwenye msongo mkubwa wa mawazo ambapo kila unapo tumia muda wako ndivyo unavyo kuwa na maisha magumu zaidi,
Sasa kipi bora kusihi misingi ya mafanikio au kutafuta siri huku ukiwa na maisha magumu zaidi ya jana bila shaka jibu unalo wewe kwa sababu nimesha kuweka wazi kila kitu kwenye makala hii.

Kila la kheri rafiki yangu,
Mwisho kabisa Nichukue nafasi hii kukukaribisha wewe rafiki yangu kwenye Programu maalumu kwa watu maalumu 2018,
Nimebakiwa na nafasi chache sana kwenye programu hii na kwa bahati nzuri sana ni kwamba wewe rafiki yangu ni mmoja wa watu wanao takiwa kunufaika na programu hii 2018.
Karibu sana niweze kukufundisha na kukusimamia kwa karibu zaidi kwa kila hatua unayo kuwa unachukua kwa mwaka mzima.
Kupata maelezo zaidi wasiliana nami moja kwa moja kwa 0715222989 WhatsApp/errynine6@gmail.com

Rafiki/Kocha&Mshauri wako
Ernest Lwilla
2018 tupige hatua pamoja.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top