Unknown Unknown Author
Title: Zijue Fikra 2 Pekee Zinazo Kuzuia Kupiga Hatua Kwenye Chochote Unacho Fanya Na Namna Ya Kuondokana Na Fikra Hizo.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki yangu? Kila siku ni zawadi  hakuna heshima inayo zidi Uhai hivyo kila pumzi ni zawadi kwako rafiki yangu. Hongera kwa siku h...

Habari rafiki yangu?
Kila siku ni zawadi  hakuna heshima inayo zidi Uhai hivyo kila pumzi ni zawadi kwako rafiki yangu.

Hongera kwa siku hii nzuri sana ambayo kwetu ni kama zawadi ya pekee na wajibu wetu ni kwenda kutumia vizuri muda tulio nao ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu ya mafanikio.
Binafsi ninaishi msingi wa NIDHAMU,UADILIFU NA KUJITUMA Je wewe unaishi msingi gani?

Karibu tena kwenye makala yetu ya leo,
Ambapo nitakwenda kukushirikisha mambo au fikra mbili ambazo zimekuwa ni kizuizi kwa watu wengi kuweza kupiga hatua kwenye maisha yao Kifikra,kifedha,kifamilia na kila eneo la maisha yao.
Watu wengi wamekuwa na mtizamo na fikra tofauti juu ya juhudi mbalimbali wanazo kuwa wanaweka kwenye maisha yao pale zinapo shindwa kuwa na matokeo yale wanayo kuwa wametarajia kupata hapo wengi kuna mambo mawili huwa ni kipaumbele kwao kufikiria na kufikiria huko ndio kinakuwa kizuizi kikubwa zaidi kwao kupiga hatua.

Fikra ya kwanza mtu kufikiria pale mambo yanapo kwenda tofauti au kuto pata matokeo ya juhudi zile anazo weka kwenye maisha yake ni USHIRIKINA.

Ndiyo,
Ushirikina ndio fikra inayo fikiriwa  na wengi pale mambo yanapo kwenda hivyo tofauti na matarajio yao,
Wengi huwa wanafikiri kwamba kuna watu wanao wafanyia ushirikina na hiyo kuwa sababu kubwa kwao kushindwa kupiga hatua.
Ukweli ni kwamba pale unapo ona mambo yanakwenda hovyo na kufikiria kuwa kuna ushirikina kwenye hilo hapo wewe ndio mshirikina kwa sababu hujataka kuisumbua akili yako kwa lolote zaidi kufikiria ushirikina.

Rafiki,
Fikra hii ya Ushirikina ni aina ya hofu nanidalili kubwa ya ujinga kwa mtu anae lifikiria hilo.
Hivyo pale unapo anza kuufikiria ushirikina tu tayari umesha jiweka na kujipa hofu ndani yako na hapa huwezi kufikiri chochote wala kutafuta tatizo zaidi.

Ushirikina ni sehemu mbaya zaidi ambapo unaitoroshea akili yako wakati wa nyakati ngumu kwenye hatua unazo chukua kila siku,Unapo fikiri hilo basi huwezi kupata mawazo ya tofauti wala kupata kiini cha tatizo hilo,Huwezi kufanya udadisi tena,Huwezi kutafuta suluhisho tena.
Mbaya kuliko ni pale unapo anza kuchukua hatua juu ya tatizo hilo hapo ndio utahisi umelogwa kwa sababu mambo yatakuwa magumu zaidi kwa sababu hukufukiria chochote zaidi ya ushirikina.

Fikra na mtizamo wa pili ambao watu imekuwa rahisi kwao kufikiria pale mambo yanapo kwenda hovyo ni CHUKI.

Ndiyo,
Chuki ni kitu cha pili kufikiriwa pale mambo yanapo kwenda hivyo na mambo kwenda tifauti na matarajio yao,
Hapa wengi huanza kutafuta mtu wa kumpa lawama,Kutupia lawama juu ya mambo hayo kwenda hovyo.

Kama unahisi kuna watu wanao husika na wewe kupata matokeo ya hivyo na hivyo kuanza kushughulika nao kwa namna yoyite ile hapo ndio unajizuia kabisa kupiga hatua kwa sababu wale wale unao fikiri wanahusika na hilo nao wanachangamoto zao kubwa na muda wote wanafikiria ni kwa namna gani wata toka kwenye changamoto hizo.
Hivyo unapo anza kuweka au kufikiri kuna watu wanao kuwekea chuki kwa namna yoyite hapo ndio unakuwa unajizuia kupiga hatua kwenye maisha yako na hivyo huwezi kupiga hatua kabisa kwa kujipa hofu na ujinga.

Mwisho kabisa rafiki yangu,
Watu wanao fanikiwa hawana hofu wa ka hawana ujinga wa aina hii na hiyo ndio sababu wanapata njia zaidi kwenye kila hatua wanayo chukua kwenye maisha yao,
Muhimu unatakiwa kufahamu kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ushirikina na mafanikio,Hakuna mtu anae fanikiwa kwa kuwa mshirikina na hivyo unapo pata mawazo ya ushirikina kama kikwazo kwako kupiga hatua jiulize kwanini ufikiri ushurikina?
Kwanini usijiulize wewe ni kwa namna gani umechangia kupata matokeo hayo? Ni kwa kiwango gani unechangia?

Chukua muda na kujihoji vizuri na kwa ukaribu zaidi kwenye eneo hilo,
Usiruhusu akili kufikiria kwa kirahisi kwenye jambo lolote unapo rahisu akili Ifikiri hivyo hapo tayari wewe unakuwa mshirikina au mwenye chuki hivyo unakuwa tayari umejitia hofu na hivyo umesha jiloga na hauwezi kufikiri tena juu ya jambo lolote.

Mwisho kabisa naendelea kukusisitiza rafiki yangu kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya ushirikina na mafanikio kwa watu wanao fanikiwa na hata wenye mafanikio makubwa.

Nichukue nafasi hii ya pekee kabisa kukukaribisha kwenye Programu maalumu kwa watu maalumu 2018,
Kama ambavyo nilikwambia rafiki yangu kuwa Nimebakiwa na nafasi chache za watu kuweza kufanya kazi na mimi moja kwa moja kwa kuwa fundisha na kuwa simamia kwenye juhudi wanazo kuwa wanaweka kwenye maisha yao.
Ninahakika kubwa hauta jitia kujiunga na programu hii muhumu zaidi kwako.
Kupata maelezo ya kina wasiliana nami moja kwa moja kupitia Mtandao wa WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com

2018 hatua kubwa ni matokeo ya juhudi tunazo weka kila siku.

Rafiki/Kocha&Mshauri wako
Ernest Lwilla.
Call/Sms 0742962058.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top