Habari rafiki yangu?
Umejizuia mwenyewe wala hakuna alie kuzuia wewe kupiga hatua kuelekea utajiri mkubwa,
Umekosea uchaguzi.
Ni imani yangu kubwa kwamba ni mzima wa afya njema na unaendelea vema na mapambano na kuweka juhudi kubwa kila siku ili uweze kupata matokeo makubwa,
Kwa hakika umechagua fungu jema kwasababu hakuna namna itakayo kuwezesha wewe kupiga hatua kubwa pasipo wewe kuweka kazi,kuweka juhudi,maarifa na hata ujuzi.
Nichukue nafasi hii ya pekee sana kuweza kukukaribusha wewe rafiki yangu kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu sana na hatua unazo paswa kuchukua dhidi ya maisha yako ili uweze kupiga hatua zaidi kuelekea mafanikio makubwa.
Nianzie hapa kwamba rafiki maisha ni yako na hivyo uchaguzi ni wako pia,
Unacho kipata ndicho ulicho kichagua na kukiwekea juhudi na iwapo unacho kipata hukitaki basi unanafasi cha kufanya uchaguzi tena na kuhakikisha unapata kile unacho kipata.
Nasema haya kwa sababu watu wengi wanaishi maisha wasiyo yataka waweza kusema wamechaguliwa na watu wengine na kwamba sasa utaishi maisha haya lakini ukweli ni kwamba wamefanya chaguzi wao na hivyo wanapo walalamikia wengine ni kujidanganya zaidi.
Rafiki chochote kinacho tokea kwenye maisha yako kiwe ni kile unacho kitaka au usicho kitaka wewe ndie ulie kivuta na hivyo iwapo unataka kuachana na kitu hicho kwa hakika uwezo wa kufanya hivyo upo ndani ya uwezo wako wewe,
Chaguzi ni mbili maisha bora au maisha yasiyo bora.
Unapo chagua maisha bora na yatofauti sawa na kuchagua kuchukua hatua kubwa na zisizo na kawaida Wakati huo huo unapo chagua maisha usiyo yapenda ni kuamua kufanya kwa ukawaida na kwa kiwango ambacho kila mmoja anauwezo wa kufanya kitu hicho na hiyo otakupa matokeo ya hovyo.
Swali pekee unalo takiwa kujihoji ni hili Je unacho kipata ni kile unacho kitaka?
Je juhudi unazo weka zinakupa kile unacho tarajia kupata?
Bila shaka utaona ni kwa namna gani uchaguzi wako ni sahihi au sio sahihi na kama utaona sio sahihi basi unanafasi ya kufanya uchaguzi tena na kuweka juhudi kwenye hilo.
Mawazo na akili zako zina nguvu kubwa sana na mchango mkubwa kwako katika kupata hicho unacho kipata kwasasa,
Hivyo iwapo unataka kupata zaidi badili mbili na uchaguzi wa kukifanya kitu unacho kifanya.
Maisha yanakupa uchaguzi wako na hakuna mtu anae weza kukulazimisha kufanya uchaguzi usio utaka wewe,
Kama biashara unayo ifanya inakupa faida isiyo kidhi mahitaji yako ya muhimu basi unachaguzi mbili muhimu kubadilisha baishara hiyo au kuona ni kwa namna gani utafanya ili iweze kukulipa,
Kama upo kwenye ajira na malipo yake hayakupi mahitaji muhimu basi unanafasi ya kuachana na ajira hiyo au kubadilisha au kufanya kwa ubora zaidi ya vile unavyo fanya sasa.
Kama kazi unayo ifanya haikupi maisha unayo taka basi unaweza kufanya uchaguzi mwingine wa kazi au kubadilisha kazi.
Mpaka hapo unaona ni kwa namna gani unauchaguzi wako kwenye kila eneo la maisha yako,
Hivyo chochote na popote unaweza kuwa bora zaidi Au kuwa hovyo zaidi.
Je unapata kile unacho kitaka?
Je unalipwa kiwango unacho stahili kulipwa?
Je unafanya kwa upendo wa thati wa moyo wako?
Je unafurahia uchaguzi wako?
Kwa maswali hayo yote kama jibu lako ni NDIYO basi endelea kuweka juhudi kubwa zaidi na kama majibu ni HAPANA basi fanya mabadiliko haraka sana kuhakikisha unapata kile unacho kitaka.
Changamoto kubwa ni kwamba huwezi kutoka hapo ulipo sasa pasipo kutambua mapungufu na hata manyanyaso ya wewe kuwepo hapo,
Hivyo kabla hujaanza kufikiri kuchukua hatua zaidi za kutoka hapo unatakiwa kutambua kwanini utoke hapo au kwanini unatakiwa kuhama hapo ulipo sasa.
Ukisha pata sababu na mbili nzuri utakazo tumia kutoka hapo sasa unaweza kuchukua hatua juu ya hilo.
Ushauri wangu kwako usifanye maamuzi ya haraka hata kama sehemu ulipo unachukizwa napo na hivyo anza kufanya maandalizi makubwa yatakayo kuwezesha kutoka hapo bila changamoto yoyote kwako,
Kama upo kwenye ajira basi unaweza kuona ni kwa namna gani utatoka hapo na kama utaenda kufanya biashara basi anza biashara hiyo ukiwa bado kwenye ajira yako,
Kama unafanya biashara usiache biashara hiyo bila kujua kwa hakika utafanya nini baada ya kuacha biashara hiyo kwa kufanya hivyo unakuwa salama zaidi kwenye maisha yako.
Kila
Ulipo umechagua kuwa na ukitaka kutoka hapo ni lazima ufanye machaguo zaidi.
Mwisho kabisa Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye Programu maalumu kwa watu maalumu 2018,
Ambapo nilitangaza nafasi chache kwa watu wachache mimi kuweza kuwa mwalimu na kiongozi wao kwenye baadhi ya maeneo ya maisha yao na hivyo bado nimebakiwa na nafasi chache ambazo wewe rafiki yangu unaweza kuzitumia kujifunza na mimi kukusimamia kwa ukaribu zaidi,
Hapa tunapata nafasi nzuri ya kushirikiana kwa karibu sana kuweza kutatua changamoto unazo zipitia,Nitakufundisha maarifa mbalimbali yatakayo kuwezesha kupiga hatua zaidi.
Kupata ufafanuzi zaidi ya program hii kwa mwaka mzima wasiliana nami moja kwa moja WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com
Kocha na Mshauri wako
Ernest Lwilla
2018,Mafanikio makubwa ni matokeo ya juhudi kubwa zaidi.
Karibu sana rafiki yangu.
Chapisha Maoni