Unknown Unknown Author
Title: Acha Kufanya Kitu Hiki Unajitesa BURE,Na Kukosa Fursa Ya Kuishi Maisha Bora.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Habari rafiki yangu? Kila mmoja anatafuta maisha ya mafanikio, Lakini ni wachache wanao fanikiwa na kuishi mafanikio yao kwa furaha. Ni i...

Habari rafiki yangu?

Kila mmoja anatafuta maisha ya mafanikio,
Lakini ni wachache wanao fanikiwa na kuishi mafanikio yao kwa furaha.

Ni imani yangu kubwa kwamba ni mzima wa afya njema na unaendelea kuweka juhudi zaidi kila siku kwenye shughuli ulizo chagua kufanya ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yako,
Na hiyo ndio njia pekee ya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yako japo uwapo katika hatua za uwekeji wa hatua hizo utapata sababu nyingi na fursa nyingi zinazo onyesha njia rahisi zaidi ya hiyo unayo itumia na kitu unacho takiwa kutizama kwenye hali hiyo ni Thamani unayo toa kwa wengine ndipo ulipwe na kama hakuna thamani unayo toa kwenye maisha ya wengine jua hakuna fursa hapo kaa mbali na habari hizo.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye makala yetu ya leo ambapo nitakwenda kukushirikisha somo zuri nililo kuandalia mimi rafiki yako,
Nina hakika kubwa sana kuna kitu kikubwa sana utaenda kujifunza na iwapo utakifanyia kazi basi utaishi maisha bora na yenye mafanikio makubwa zaidi pasipo kuwa na tatizo lolote.

Janga kubwa kwa watu wengi sio mafanikio japo hilo nalo ni tatizo lakini ni kwa kiwango fulani lakini Janga kubwa ni watu kuishi maisha yenye furaha,
Ndiyo furaha,Nasema hivi kwa sababu kama mafanikio kuna watu wanamafanikio makubwa sana lakini bado mafanikio hayo ni mzigo mkubwa sana kwao.

Ukiachana na hilo pia Wapo watu wanao kuwa na maisha bora lakini bado hawayafurahii maisha hayo na hicho ni kitu kinacho pelekea kwa watu wasio kuwa na mafanikio kuona bora waendelee kuishi maisha hayo kwa sababu iwapo watafanikiwa basi watakuwa wamejiingiza kwenye matatizo ya watu wenye mafanikio makubwa ambapo wengi hawaishi maisha yenye furaha.

Labda nikuulize kitu wewe rafiki yangu juu ya hili,
Kipi ni bora kati ya kuwa na mafanikio makubwa alafu ukakosa furaha au kuwa na maisha ya furaha lakini ukiwa hauna mafanikio yoyite hasa ya kifedha?

Hapo jibu la wengi litakuwa bora niishi bila mafanikio lakini nikiwa na furaha kwa sababu ndio maisha walio zoea kuishi.
Hivyo kwenye makala hii nitakwenda kukushirikisha jambo muhimu litakalo kupa furaha na huku ukiwa na mafanikio makubwa pasipo mafanikio hayo kuwa mzigo kwako.

Jambo pekee linalo pelekea watu wengi kuishi maisha ya mafanikio huku wakiwa hawana furaha ya kuishi mafanikio hayo ni KUWEKA FURAHA KWENYE VITU,
Nielewe vizuri hapo kwamba mtu anamiliki gari na kisha anaweka furaha yake kwenye gari hilo analo limiliki,Mtu anamiliki fedha nyingi na kisha anahamishia furaha hiyo kwenye fedha zake,Mtu anamiliki nyumba nzuri basi anahamishia furaha yake kwenye vitu hivyo.

Kwa njia hiyo mtu huyu anakuwa hana furaha mpaka anapo kuwa na kitu hicho,
Mtu hawezi kuwa na furaha wala Amani anapo kuwa mbali na vitu hivyo.
Sasa huu ni upande wa watu wenye mafanikio wakati upande wa pili ni watu wasio na mafanikio na wanakuwa hawana vitu hivyo vyote hivyo furaha yao ni  zawadi ya uhai walio nao.

Rafiki hakikisha ulipo ndipo furaha yako ilipo,Usiweke furaha yako kwenye vitu ambavyo upo wakati utakuwa navyo mbali au utavipoteza kufanya hivyo ni kujitengenezea matatizo zaidi,
Usiweke furaha yako kwenye magari na mali mbalimbali unazo miliki hata kama ni kitu kidogo mfano wa simu usiweke furaha yako kwenye kifaa hicho kwa sababu kuna wakati utalazika kuwa mbali nacho na hivyo utaipoteza furaha yako ya kufurahia mafanikio uliyo nayo.

Hii haina maana uishi kama hauna vitu hivyo hapana,Ninacho maanisha hakikisha havikutawali au havichukui hisia za furaha yako kwa sababu iwapo itakuwa hivyo ni hatari zaidi hasa pale inapo tokea umepoteza.

Mfano:Umeweka furaha yako kwenye mahusiano ya mapenzi na kuamini kwamba wewe huwezi kuishi bila unae mpenda,
Hapo furaha yako unakuwa umeiweka kwenye mapenzi sasa changamoto ni pale inapo tokea upo mbali na mahusiano yako au mahusiano yako yameingia kwenye changamoto.
Hapo ndipo watu huona haina maana kwao kuwa na mafanikio kwa sababu mafanikio hayo yanakuwa hayana maana pasipo uhusiano wao wa mapenzi.

Au hata unapo weka furaha yako kwenye fedha na hivyo kuitumia fedha yako kama chanzo kikuu cha furaha sasa changamoto inakuja pale unapo kosa uhakika wa kuwa na fedha muda wote na mbaya zaidi ni pale unapo poteza fedha hizo na hivyo kushindwa kabisa kuishi maisha ya furaha kwa sababu furaha yako ipo kwenye fedha na fedha hauna umeona hapo rafiki inavyo kuwa sasa?

Nini ufanye rafiki yangu kama hutakiwi kuweka furaha kwenye vitu?
Jambo unalo takiwa kulifahamu na kulisimamia ni kuhakikisha ulipo wewe ndipo furaha yako inapo kuwa,
Yaani wewe uwe ndiye furaha mwenyewe.

Kwa njia hii hata usipo kuwa na chochote kwa wakati huo unakuwa na furaha ya kutosha sana.
Mfano:Kipindi cha nyuma nilikuwa nikishindwa kabisa kuishi maisha ya furaha nikiwa sina fedha,Sina bidhaa dukani na hivyo inapo tokea sina vitu hivyo basi ninakuwa nahisi ndio mwisho wa maisha yangu,Naona kama hakuna njia nyingine tena itakayo fanya maisha yangu kuwa bora.
Lakini ubaya zaidi ni pale hali hiyo inapo nizuia hata kufanya maamuzi bora au kufikiri kitu kwa kina na kukitolea maamuzi yaliyo sahihi.
Sasa kwa njia hiyo unaona nikwanamna gani najinyima fursa nzuri ya kufurahia uhai nilio nao,Kufurahia Fahari ya kufikiri kwa kina,Kufahari ya kufanya maamuzi sahihi n.k na mbaya zaidi muda mwingine hata kama kitu kinge kuwa cha kawaida basi nakuwa na hasira kama ni jambo kubwa sana hapo ndipo nilipo ona ni kwa namna gani hali hiyo inanizuia kuishi maisha ya furaha ya maisha yangu.

Bila shaka umesha ona ni kwa namna gani furaha inaweza kutoweka iwapo utakosa vitu vilivyo itawala hisia hiyo ya furaha,
Kuwa furaha ya wewe na miliki mafanikio makubwa zaidi na usichanganye na kuweka furaha yako kwenye vitu.

Mwisho kabisa Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye Program Maalumu kwa watu maalumu 2018,
Ambapo unapata fursa nzuri sana ya kujifunza na kushirikiana na mimi rafiki yangu moja kwa moja.
Hapo tutajifunza na kuchukua hatua na kusimamia hatua zetu pamoja nami nikiwa kocha wako yaani mtu wa karibu zaidi kwako kihatua za mafanikio.
Kupata maelezo zaidi ya namna ya kujiunga na programu hii wasiliana nami moja kwa moja kupitia Mtandao wa WhatsApp 0715222989/errynine6@gmail.com

Kocha na Mshauri wako
Mwandishi/Mjasiriamali na Mshauri wa Biashara.

Ernest Lwilla.
2018 Mafanikio ni matokeo makubwa ya hatua tunazo chukua kila siku.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top